Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

June 25, 2013

MARALIA NA MFUMO WA HEWA VYAONGOZA KWA KUUA WATOTO LUDEWA.



             
UGONJWA wa malaria na mfumo wa hewa vimetajwa kuongoza kwa vifo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe huku ushirikina na matumizi mabaya ya vyandarua vikitajwa kuwa vyanzo vikuu vinavyosababisha kuongezeka kwa vifo hivyo.

Akizunguza jana ofisini kwake mratibu wa maralia wilayani Ludewa Kelvin Mfuse alisema kundi linaloongoza kwa vifo ni watoto wadogo chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito na wazee pamoja na waathrika wa virusi vya ukimwi ambao kinga zao za mwili zimepungua.

’’’’ hali halisi ya maambukizi ya malaria kiwilaya katika magonjwa kumi ambayo yalijitokeza kwa wagonjwa wan je (OPD) malaria inaonekana inqonekana iko namba mbili ikianza ugonjwa wa mfumo wa hewa.’’’’ Alisema Mfuse

Mfuse aliyataja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na Nimonia,kuharisha, upasuaji mdogo,magonjwa ya ngozi, macho, ajali na magonjwa mengine, mfumo wa hewa na malaria inayoongoza kwa vifo 59 kati ya vifo 158 ya vifo vilivyotokea kwenye vituo vya kutolea hauduma sawa na asilimia 37 ya vifo kwa kipindi cha mwaka jana.

Aidha mratibu huyo alifafanua kuwa wagonjwa 8248 walio chini ya miaka mitano kati ya wagonjwa 31,916 waliokuja kutibiwa walikuwa na malaria na wagonjwa wa malaria wenye umri zaidi ya miaka mitano 13,608 walikuwa na malaria kati ya 41,394 sawa na asilimia 29  ya wagonjwa wote.

Dr Mfuse alizitaja sababu zinazopelekea kupanda kwa vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria kuwa ni pamoja na jamii kutokutumia vyandarua vilivyotolewa na serikali kwa visingizio mbalimbali ikiwemo madai kuwa vyandarua hivyo hupunguza nguvu za kiume.

Sababu zingine ni wananchi kutumia vyandarua kwa matumizi yasiyorasmi kama vile kuvulia samaki katika ziwa nyasa badala ya kutumia kuzuia mbu huku wengine wakitumia vyandarua hivyo kufugia kuku majumbani.

Kauli mbiu ya siku ya malaria mwaka huu wekeza kwa maisha yako ya baadaye kutokomeza malaria.

Hata hivyo kasi ndogo ya kupambana na malaria katika wilaya ya Ludewa inasababishwa na changamoto kadhaa ikiwemo jamii kukosa elimu juu ya matumizi sahihi ya vyandarua, ufinyu wa bajeti kwa ajili ya kufikia malengo na uhaba wa watumishi hasa wale wenye sifa za kitaaluma.

Wilaya ya Ludewa imegawanyika katika kanda au maeneo makuu matatu ikiwemo ukanda wa juu sehemu ya milimani ambako wanaamini hakuna malaria kutokana na hali ya hewa ya ubaridi, sehemu ya ukanda wa kati ambao maambikizi yake ni wastani na ukanda wa chini ambao maambukiza yake ni makubwa sababu ya kuwa na mazalia ya mengi ya mbu.
           mwisho

No comments: