ONGEZEKO la wanafunzi
wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu katika wilaya ya Ludewa linasababishwa na
watoto kuanza elimu wakiwa na umri mkubwa lakini pia linachangiwa na walimu
kukaa muda mrefu bila kupata mafunzo mahali pa kazi.
Hayo yamebainishwa na
shirika lisilokuwa la kiserikali la kitaliano la ACRA linalofanya miradi
mbalimbali ya kijamii wilaya Ludewa katika Mkoa wa Njombe katika utafiti wake
juu ya nini chanzo cha ongezeko la watoto wanaohitimu elimu ya msingi huku wakiwa
hawajui kusoma, kuandika wala kuhesabu.
Akizungumza katika warsha ya siku moja kwa
maafisa elimu sekondari na msingi, walimu na wadau mbalimbali wa elimu meneja
wa shirika hilo Beppe Buscaglia alisema madhumuni ya warsha ni kukutana na
wadau wa elimu na kujadili kwa pamoja juu ya mustakabali wa elimu na changamoto zake wilayani Ludewa.
Beppe alisema shirika
lake limefanya mambo mengi wilayani Ludewa ikiwa ni pamoja na ujenzi na
ukarabati wa madarasa na nyumba za walimu kutokana na shule nyingine kuwa na
vyumba vya madarasa ambavyo ama ni vibovu au vimechakaa.
Buscaglia akaongeza
kuwa matokeo na mafanikio ya shirika la acra kuwagharimia mafunzo walimu
kupitia chuo cha uwalimu cha Kreruu cha mjini Iringa kumeleta ufanisi mkubwa kwa
walimu hao ikiwa ni pamoja na ongezeko la ufaulu na mahudhurio mazuri kwa wanafunzi.
Shirika hilo
linalofanyakazi wilayani Ludewa limegundua kuwa watoto wengi wa kitanzania
wanashindwa kumudu masomo kutokana na kukosa msingi wa elimu wakiwa wadogo na
baadaye kurundikiwa mzigo mkubwa wa masomo wanapoanza darasa la kwanza na
kuchanganyikiwa na kasha kuamua kuacha shule.
Ni kutokana na
kuporomoka kwa elimu nchini, shirika lisilo kuwa la kiserikali la ACRA limeamua
kuwapeleka mafunzo ya muda mfupi walimu wa shule za awali wasio na ajira
serikalini na walimu wa shule za msingi wenye ajira kutoka kata za Mawengi,
Milo na Mlangali wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe ili waweze kufanyakazi
zao kwa ufanisi.
Shirika hilo
linalofanyakazi wilayani Ludewa limegundua kuwa watoto wengi wa kitanzania
wanashindwa kumudu masomo kutokana na kukosa msingi wa elimu wakiwa wadogo na
baadaye kurundikiwa mzigo mkubwa wa masomo wanapoanza darasa la kwanza na
kuchanganyikiwa na kasha kuamua kuacha shule.
Hadi sasa shirika la
ACRA limeshawapeleka mafunzo walimu 65 katika chuo cha ualimu cha Kreluu ambapo
kati yao walimu 52 wanatoka katika shule za msingi na walimu 13 wanatoka katika
shule za awali ambao hawana ajira serikalini.
Sababu zingine
zilizotajwa na ACRA kama tatizo katika mfumo wa elimu ni pamoja na walimu kukaa muda mrefu kazini bila kupata
mafunzo ya mara kwa mara ili kwenda na wakati na walimu wa msingi kupewa
kufundisha madarasa ya awali bila kuwa na mafunzo katika ngazi hiyo.
Naye Robert Hyera
afisa elimu msingi wilaya ya Ludewa aliyealikwa kama mgeni rasmi, akifungua
warsha hiyo alikiri kuwepo kwa wimbi la walimu waliokaa zaidi ya miaka kumi tangu kuhitimu vyuoni ambao hadi sasa hawajawahi
kupata mafunzo wala semina yoyote jambo ambalo linatishia kudidimiza elimu kwa
sababu walimu hawaendi na wakati.
“”” walimu wanahitaji kupata mafunzo ya mara
kwa mara ili kwenda na wakati tena sambamba na mitaala lakini pamoja na
kuyakabili mabadiliko yanayokea kila siku katikasekta ya elimu nchini.’’’’’
Alishauri Hyera
Aidha Bw Hyera
alilisifu na kulipongeza shirika la acra kwa kugundua mapungufu hayo ambayo
kimsingi kutokumwendeleza mwalimu ni kumdidimiza mwanafunzi kielimu na kwamba
kama serikali itaiga mfumo huo basi itakuwa imeondoa na kufuta kabisa kuwepo
kwa watoto wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu.
“’’’’ tumekuwa na
matatizo katika idara ya elimu kutokana na bajeti finyu ambayo imepelekea
kudorora kwa elimu kwani walimu walio wengi hawapati mafunzo ya mara kwa mara
ili kuboresha ujuzi na taaluma zao jambo ambalo linasababisha matokeo mabovu
kwa wanafunzi”,akaongeza Bw.Hyera.
Katika mradi huo
walimu wawili wa madarasa ya awali kutoa Ulayasi na Mlangali ambao wanajitolewa
pasipo kuajiriwa serikalini walipata mafunzo ya miezi mitatu katika chuo cha ualimu
Kreluu walipata mafunzo ya miezi mitatu na kuona mabadiliko makubwa.
Kwa upande wao walimu
Tulamvona Mturo wa shule ya msingi mlangali na Imelda Cassian Mtweve mwalimu wa shule ya
awali ulayasi ambaye analipwa na jamii alisema mafunzohayo yamemsaidia na
kumwongezea maarifa sana.
‘’’’’ kabla ya kupata
mafunzo alikuwa akiingia darasani na kuanza kufundisha moja kwa moja bila ya
kuwapa wanafunzi muda wa kucheza. Lakini kupitia mafunzo niliyoyapata nimeweza
kuelewa saikolojia ya watoto na imekuwa rahisi kulimudu darasa kutokana na
kuzitambua tabia tofauti za wanafunzi anaowafundisha.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment