MAHAKAMA
ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe imemhukumu kwenda jela miezi kumi na
mbili na kunywang’anywa leseni ya udereva na kisha kufungiwa kutoendesha gari
lolote katika maisha yake Edward Mliwa kwa kusababisha majeraha kwa watu watano
baada ya kupata ajali kwa uzembe.
Akisoma
hukumu hiyo iliyochukua takribani masaa mawili hakimu mkazi mfawidhi wa
mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna alisema kuwa mahakama yake
imeridhika na ushahidi ulioletwa mbele yake na upande wa mashtaka na kwamba
mshtakiwa atatumikia kifungo cha miezi kumi na mbili jela au kulipa faini ya sh
hamsini elfu (50,000) kwa kila kosa.
Lukuna
mshtakiwa Edward Mliwa anashtakiwa kwa makosa matano ikiwemo kuendesha chombo
cha moto kwenye barabara ya umma kwa uzembe na kusababisha ajali iliyowajeruhi
watu watano kinyume na sheria chini ya kifungu 41, 50 na 63(2) cha sheria
barabarani sura ya 168.
Hakimu
mkazi mfawidhi akaendelea kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Novemba 12 mwaka
2012 katika kijiji cha Masasi barabara ya Ludewa Manda wilayani Ludewa ambapo
alikuwa akiendesha gari aina ya center yenye namba za usajiri T 715 AZU akiwa
amebeba abiria kupita kiasi.
Awali
mshtakiwa alikiri kosa moja tu ambalo ni kusababisha majeraha kwa abiria watano
lakini akakana kuhusika na kosa na uzembe akiwa na chombo cha moto hata hivyo
mahakama hiyo imeiamuru mamlaka ya mapato nchini TRA kuifungia leseni ya
mshtakiwa maisha kutokana na makosa hayo.
Akiomboleza
mahakani hapo Edward Mliwa akaiomba mahakama kumwonea huruma na kumpunguzia
adhabu kwa sababu anayofamilia inayomtegemea, hata hivyo alilipa faini na
kupona kwenda jela.
Mwisho
No comments:
Post a Comment