WANANCHI wa kijiji cha Ludewa (K)
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe wametishia kugoma kutoa michango pamoja kutojihusisha
na shughuli za maendeleo kijijini hapo kama uongozi utashindwa kutoa
taarifa ya mapato na matumizi haraka.
Hatua hiyo imekuja kutokana na
uongozi kushindwa kuitisha mkutano wa hadhara kijijini hapo kwa ajili ya kutoa
taarifa ya mapato na matumizi na kupelekea wananchi kukosa imani na uongozi huo
akiwemo mwenyekiti wa serikali ya kijiji Dizbody Nkinga na afisa mtendaji wake
Oraph Kiowi.
Wakizungumza jana kwa nyakati
tofauti wananchi hao walisema kwa mara ya mwisho mkutano kwa ajili ya kusoma
taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji chao ilitolewa julai 2 mwaka jana
ambapo hata hivyo taarifa haikuwa ya kuridhisha ilikuwa na mapungufu mengi.
‘’’’ sisi wananchi tunaendelea
kutozwa michango mbalimbali kila kukicha kijijini hapa lakini hatuelewi
viongozi wetu wamekusanya mapato kiasi gani na matumizi yaliyofanyika hali
ambayo inatukatisha tamaa kabisa ni bora tuache kuchangia shughuli za maendeleo
kutokana na kutokuwa na uwazi katika makusanyo na matumizi.’’’’ alisema mkazi
wa kijiji hicho ambaye hakupenda jina lake liandikwe
Aidha afisa mtendaji wa kijiji hicho
Bw.Oraph Kiowi alikili kuwa ofisi yake haijaweza kuwasomea wananchi taarifa za
mapato na matumizi kwa muda mrefu hivyo wananchi hao wanahaki ya kuulalamikia
uongozi wa kijiji hicho.
Kiowi alisema tatizo la kutosoma
taarifa hizo ni kutokana na ushirikiano mdogo anaoupata kutoka kwa wenyeviti wa
mitaa ambao ni wajumbe wa halmashauri ya kijiji kwa kutohudhuria katika vikao
vya ndani kila anapoitisha vikao hivyo.
Nae mwenyekiti wa kijiji hicho
Disbody Nkinga alisema kumekuwa na kutoelewana kati ya wenyeviti wa mitaa na
afisa mtendaji wa kijiji hivyo kusababisha kukwamisha shughuli za maendeleo
kutokana na wenyeviti hao kushindwa kufanya kazi zao.
Nkinga alisema mwaka 2012
alimuandikia barua na kumjulisha mtendaji wa kata ya Ludewa kuhusiana na tatizo
la wenyeviti hao wamitaa na wajumbe wa halmshauri ya kijiji kutohudhuria vikao
vya ndani ili kuweza kuwasomea wananchi taarifa za mapato na matumizi na
kushindwa kukusanya michango ya maendeleo.
Maamuzi yaliyofanyika na ofisi ya
kata ilikuwa ni kuwachukulia hatua za kisheria ambapo majina yao yalifikishwa
mahakamani na wakatakiwa kwenda kijibia mahakamani lakini wenyeviti hao
walitoroka na kwenda kusiko julikana,na mpaka sasa wengine wanaendelea na kazi
lakini bado tabia yao ya kutofuatilia michango inaendelea.
Bw.Nkinga aliwataka wananchi kuwa
waangalifu wanapochagua viongozi wa mitaa richa ya wananchi hao kuushutumu
uongozi mzima wa kijiji kuwa unashiriki katika kudidimiza maendeleo ya kijiji
hicho kwa kutafuna michango ya wananchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment