Haya ndio maporomoko ya mto Lupali wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ambako umeme utazalishwa na shirika la LCBA na kusambazwa zaidi ya vijiji 19
Baadhi ya wajumbe wa shirika hiilo wakiangalia maporomoko ya mto Lupali
Wajumbe wa LCBA wakiiwa na wataalamu katika upimaji
misitu iliyoko katika mto Lupali
wajumbe wakiwa na wataalam wa masuala ya Ardhi
misitu ya mto Lupali
VIONGOZI wa vijiji
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wametajwa kuwa kikwazo cha uharakishaji
wa mradi wa umeme unaotarajiwa kuzalishwa katika maporomoko ya mto Lupali kata
ya Mundindi kutokana na viongozi hao kushindwa kukusanya michango kwa wananchi.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo katibu wa shirika la Ludewa Capacity Building
Association(LCBA) Bw.Joseph Kayombo alisema zoezi la upembuzi yakinifu katika
vijiji zaidi ya kumi na tisa ulitakiwa kuanza june mosi mwaka huu lakini imeshindikana
kutokana na wenyeviti na watendaji katika vijiji husika kushindwa kukusanya
asilimia 20 ya fedha kutoka kwa
wananchi.
’’’’ mamlaka ya
usambazaji umeme vijijini Rular Enegy Agecy (REA) ilishatoa mwongozo juu ya
miradi hiyo ambapo kila kijiji kinatakiwa kuchangia gharama ya nguvukazi na
fedha 2% ili kukamilisha mradi huo lakini mpaka sasa baadhi ya viongozi wa
vijiji wamekuwa kikwazo kwa kushindwa kufanya kazi hiyo.’’’’’ Alilalamika Kayombo
Kayombo aliongeza
kuwa lengo la REA ni kumtaka mwananchi achangie japo kidogo ili aweze kujiona
naye ni sehemu ya mradi huo katika umiliki lakini mpaka sasa mamlaka hiyo
imeshatoa fedha za awali kinachosubiriwa ni michango ya wananchi ili kazi
ianze.
Alisema shirika lake
ndilo shirika pekee lililopewa dhamana ya kuusimamia mradi huo na tayari liko
katika hatua nzuri lakini kinachosikitisha ni baadhi ya watendaji na wenyeviti
wa vijiji kushindwa kukamilisha makubaliano ya michango ili kazi ianze.
“tulikubaliana mwisho
wa kuileta michango yao ni Mey 30 mwaka huu ili Juni 1 kazi ianze lakini mpaka
sasa viongozi hao wamekuwa wakitoa ahadi bila utekelezaji hali ambayo
inatuchelewesha kuanza kazi za mradi huo wa umeme ambao utaleta manufaa makubwa
kwa wananchi na Taifa”,alisema Bw.Kayombo.
Bw.Kayombo
alisema umeme huo unakadiliwa kutoa megawalt 30 ambazo zitavinufaisha zaidi ya vijiji
19 kwa gharama nafuu kutokana na shirika hilo kujihusisha na utoaji misaada na
elimu katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya ya Ludewa.
Alivitaja
vijiji vitakavyonufaika na huduma hiyo katika kata ya Mundindi kijiji cha
Mundindi,Amani na Njelela,kata ya Ibumi ni kjiji cha Ibumi na kata ya Madilu ni kijiji cha
Madilu,Ilininda,Ilawa,Mfalasi na Manga kata ya Madope kijiji cha Madope,Luvuyo
na Mangalanyene.
Vijiji
vingine ni Mkongobaki,Lipangala,Ugela,Shaurimoyo na Mdilidili,Mbwila na Luana
hata hivyo alisema umeme huo utakuwa na nguvu kubwa hivyo unaweza kusambaa
katika vijiji vingi zaidi itakavyowezekana kutokana na wafadhiri wa mradi huo
watakavyopendekeza.
Aidha
mjumbe wa shirika la LCBA Bw.Lazaro Mwinuka alifafanua kuwa shirika hilo
unakadiliwakutumia kiasi cha shilingi 40 Bilion kutoka Bank ya Dunia
kupitia REA ambazo zitafanya kazi zote mpaka mradi huo utakapo kamilika.
Bw.Mwinuka
alisema mchakato wa mradi huo umeshaanza lakini unatarajia kumamilika ifikapo
mwaka 2014 kutokana na ukubwa wa mradi hivyo wananchi wa vijiji tajwa
wanatakiwa kuanza maandalizi katika nyumba zao ili waweze kunufaika na mradi
huo.
Alisema kama
watendaji wa vijiji watakamilisha michango yao haraka basi mradi huo
unakamilika mapema ili kuwapa fulsa wananchi kuanza kunufaika kabla ya machimbo
ya mchuchuma na Liganga
Mwisho.
No comments:
Post a Comment