Chanzo cha maji hayo ambapo pametegwa(intake) pakiwa pamebomoka baada ya kujengwa kabla ya kuisha ujenzi wa mradi huo.
Mwananchi akiwaonesha waandishi wa habari jinsi uchanganyaji wa saruji na mchanga ulikoa chini ya kiwango ndio sababu kubwa ya kubomoka kwa bwawa hilo.
Ukuta wa bwawa la kukusanyia maji ukiwa umebomoka
kulia ni mwandishi wa mtandao huu Bw.Nickson Mahundi akiwa na wananchi eneo la ujenzi wa bwawa la kukusanyia maji kijiji Mbwila
Ukubw wa bomba lililotegwa katika chanzo hicho haukidhi viwango vya usambazaji maji kutoka intake kwenda kwa wananchi wa kijiji cha Mbwila ukilinganisha na uwingi wa wanakijiji wa kijiji hicho.
wananchi wakiangalia ujenzi wa intake hiyo ulioanza kubomoka
haya ndio maji katika mradi huo
Mwandishi wa mtandao huu akiangalia bomba zilikoelekea
Safari ya kuelekea katika safu ya milima livingstone ambako intake hiyo imejengwa
Waandishi wa habari wakitembea kwa miguu kuifuata intake hiyo
Hili ndilo bomba kuu linalotoka katika intake hiyo na kwenda kwa wananchi,ni mradi uliogharimu shilingi 243 milioni lakini bado haujakamilika kwa kusuasua kwa wakandarasi
Bomba kuu la kutoa maji intake
safari ya intake ikiwa inaendelea
Bomba kuu kutoka intake
Wanahabari wakikaribia intake
Bomba kuu la kutoka intake
misitu iliyoko safu za milima livingstone
ukuta ukiwa umebomoka
intake ikiwa imebomoka
bwawa la kukusanyia maji likiwa limejengwa lakini badop maji yanapita chini ya intake hiyo
maji yakiingia katika bwawa hilo
bomba kuu linalotoka intake
Wananchi wa
kijiji cha Mbwila wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wamemlalamikia
mkandarasi wa kampuni ya Northern Costruction ltd kwa kusuasua katika ujenzi wa
mradi wa maji ambao ni ukombozi kwa kijiji hicho.
Akitoa
malalamiko hayo mbele ya waandishi wa habari waliotembelea mradi huo mmoja wa
wananchi wa kijiji cha Mbwila Bi.Mariam Haule alisema kijiji hicho kimekuwa na
tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa muda mrefu lakini chakushangaza
Serikali imetoa fedha ili kutatua tatizo hilo na aliyekabidhiwa fedha hizo
anasuasua kujenga mradi huo.
Bi.Mariam
alisema tatizo la maji wanaopata tabu zaidi ni wanawake kutokana na umbali mrefu
wanaotembea kufuata maji hayo,wao kama wananchi walifurahia sana kitendo cha
Serikali kutopa fedha hizo lakini hata eneo la kutega maji hayo limejengwa
chini ya kiwango.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Bw.Gerod Haule alisema ujenzi wa chanzo cha maji hayo ulikuwa
ukiendelea vizuri lakini mpaka sasa ni zaidi ya miezi miwili kampuni hiyo
haionekani kijijini hapo bila ya taarifa yoyote ikiwa hata ujenzi wa awali
umeanza kubomoka.
Bw.Haule
alimtaja msimamizi wa mradi huo ambao umegharimu shilingi 243 milioni kuwa ni
George Mpilima ambaye amekuwa akiahidi kuukamilisha mradi huo ndani ya mienzi
sita lakini kwa mujibu wa mkataba wa mradi huo ni mwaka mmoja ambapo mpaka sasa
umebaki mwezi mmoja na nusu na hakuna kinachoendelea.
“Tumeshangazwa
na mwenendo wa ujenzi wa mradi huu kutokana na hata ujenzi wa eneo ambako maji
hayo yatatengwa uko chini ya kiwango na umeshaanza kubomoka kabla mradi
haujakamilika sasa bado hatuelewi ni kitu gani kinaendelea ili mradi huu
ukamilike”,alisema Bw.Haule.
Msimamizi wa
mradi huo Mhandisi George Mpilima alikili kuwa yeye ndiye msimamizi na akamtaja
mkurugenzi wa Kampuni ya Northern Contruction ltd ndiye aliyeshika ukandarasi
na kumuajiri yeye lakini kutokana na sababu zisizozuilika mradi huo umekuwa
ukisuasua lakini utakamilika.
Bw.Mpilima
alijitetea kwa kusema muda wa kukabidhi mradi huo bado haujafikia hivyo kwa
muda mwa mwezi mmoja na nusu mradi huo utakamilika na kuwataka wananchi wasiwe
na wasiwasi na kampuni yake kwani inauzoefu na kazi za namna hiyo.
Aidha
Muhandisi wa maji katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Athanasius Munge
alisema mradi huo ulioanza Julai 2012 unatarajia kumalizika Julai mwaka huu
lakini mpaka sasa hauko katika hali nzuri kutokana na mkandarasi huyo kuondoka
bila taarifa katika eneo la mradi kwa zaidi ya miezi miwili.
Bw.Munge
alisema mkandarasi huyo amekuwa msumbufu kwa kutopatikana kwa muda mrefu hata
akipigiwa simu yake ya mkononi wakati mwingine kushindwa kupokea kutokana na
kutokuwa na sababu za msingi za kusiotisha mradi huo.
“Tumekuwa
tukimtafuta na taarifa kwa maandishi nimeziwasilisha kwa mkurugenzi wa
halmashauri ambapo alimuandikia barua ya onyo Februali mwaka huu bado ni mkaidi tuansikia amekuja huko hapa
wilayani lakini tunajaribu kuangalia namna ya kufanya katika mkataba wake”,alisema Bw.Munge.
Bw.Munge
alisema hata ujenzi wa chanzo cha maji hayo(intake)unaonekana uko chini ya
kiwango kutokana bado mradi huo haujaisha ni mwenzi mmoja umebaki lakini
umeshaanza kubomoka baadhi ya kuta.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Northern construction ltd ambayo inajenga mradi huo aliyejitambulisha
kwa jina moja la Mchenya alipotakiwa kuutolea maelezo kwa njia ya simu ya
kiganjani alijibu yeye si msemaji wa
mradi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment