Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

May 04, 2013

MAJIBU YA MASWALI KUHUSU UJASIRI WA FILIKUNJOMBE BUNGENI YAMEPATIKANA.




    
                   Mh.Deo Filikunjombe

UMASKINI, shida na matatizo ya usafiri katika ziwa nyasa, barabara ya lami kutoka njombe hadi manda na ucheleweshwaji wa ujenzi wa chuo cha veta, ndivyo vinavyomkosesha amani na kumnyima uzingizi mbunge wa Ludewa katika mkoa wa njombe Deo Filikunjombe imefahamika. 

Akizungumza na kipindi hiki Filikunjombe alisema pamoja na baadhi ya wenzake kutokumwelewa kufuatia misimamo yake hajutii wala kubadili msimamo wake na kwamba yeye hawezi kuumizwa na mambo ya kitaifa wakati wananchi wa Ludewa wakiendelea kuteseka kwa kukosa mahitaji muhimu ambayo kimsingi ni haki yao haiingii akilini hata kidogo. Aling’aka

‘’’ Serikali isipo badilika mimi na wananchi wa Ludewa tupo tayari kuandamana tukiwa tumevalia mashati ya kijani na suruali nyeusi  mpaka kieleweke.’’ Kauli ya filikunjombe

Filikunjombe aliyataja mambo matatu yanayomuumiza na kumnyima usingizi na kupelekea kusimama akiwa na nguvu bila hofu bungeni kuwa ni  pamoja na  usafiri wa meli mpya katika ziwa nyasa ambayo ni ahadi ya rais pamoja na ukarabati wa meli mbili zilizopo ambazo ni chakavu, kuharakishwa kwa barabara ya lami kutoka njombe hadi manda na kuharakishwa kwa ujenzi wa chuo cha Veta ili wananchi wake wafaidi matunda ya miaka 50 ya uhuru wa nchi hii.

Wananchi wa kata ya Lumbila wao wanafuata huduma ya afya wilayani kyela mkoani mbeya ambako hutumia mitumbwi kusafirisha wagonjwa na wajawazito.’’’’ Alisema mzee Joseph Mwakasungura

DEO alikataa kuunga mkono hoja ya waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika bunge la bajeti kwa kusema serikali siyo sikivu katika mambo ya utekelezaji hasa inapobainika katika baadhi ya mambo yanayokwenda kinyume na matokeo kuwa mabaya haichukui hatua kwa viongozi na watendaji husika.

Alisema viongozi wamekuwa Wakiendelea kulindana wao kwa wao kana kwamba hawaoni kinachofanyika mbele yao  yapo mengi nitaeleza machache kwa muda huu elimu katika nchi hii pamoja na kwamba tumejenga shule nyingi za sekondari kila kata.

‘’’’’ mwaka 2012 kulikuwa na ongezeko la ufaulu wa wanafunzi wa Darasa la Saba kujiunga kidato cha kwanza tukajipongeza sana kwa matokeo hayo lakini ikagundulika ufauru huo ni pamoja na watoto wasiojua kusoma na kuandika zaidi ya elfu kumina moja na waziri mkuu akaunda tume lakini hadi sasa hatujaona kuwajibika kwa yeyote katika wizara husika,

‘’’’tena imekuwa vivyo hivyo 2013-kufeli kwa wanafunzi kidato cha nne vibaya zaidi pia tume imeundwa kuchunguza  na tunajua haitakuwa na lolote zaidi ya Funika kombe Mwanaharamu apite.’’’’ Alisema kwa masikitiko filikunjombe

Kauli hiyo Ikimaanisha tusahau mambo ya tumeiliopita  tujadili ya sasa  hukutunajua hakuna kitakacho fanyika kiutekelezaji, aidha alisema tukumbuke

Filikunjombe alisema elimu ya msingi  itolewayo katika  nchi hii  sio bure tena  kama tunavyosema bali ina gharama zinazotokana na michango mingi inayomghalimu mzazi  kwa mtindo wa michango inayojumlisha kuanzia Tsh,6000/= mpaka 12,000/= kwa mwanafunzi mmoja kwa mwaka na kwamba ni heri turudishe ada wazazi wajiandae.

Deo alionesha kushangazwa na Serikali hii ilivyokaa kimya huku ikijua  wananchi wanaona haya yote yanayofanyika na kwakupitia matatizo haya  pesa  ya umma inatumika vibaya   tena akastaajabu kuona wabunge wenzake wakigeuka kupinga kila hoja za wapinzani bila kuchunguza zinahusu nini  kwa maslahi ya wananchi.

mwisho

No comments: