Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

May 18, 2013

MKUU WA WILAYA YA LUDEWA AAPA KUTOWASAIDIA WATAKOKUMBWA NA BALAA LA NJAA WILAYANI HUMO.



Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha akihutubia wananchi siku ya familia Duniani wilayani Ludewa

viongozi mbalimbali wakifuatilia sherehe hizo
Mwalimu Frola Mgaya wa shule ya msingi songambele akipiga ngoma siku ya sherehe ya familia Duniani
Bi.Monica Mchilo ambaye ni diwani wa kata ya Ludewa akicheza ngoma ya maharamisi
 Afisa tawala wa wilaya ya Ludewa Bw.Charles Keiya akiwasalimia wananchi
kikundi cha ngoma ya mganda cha mzalendo kikitumbuiza
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha na mkurugenzi wa halmashauri ya wilya ya Ludewa Bw.Waziri wakiondoka katika sherehe hizo
 wanafamilia wakisoma risala siku ya familia
 Wanaiva youth group hao
 Mwalimu Lyuu wa shule ya msingi Ludewa Mjini akiimba katika sikukuu ya familia

Kutoka kushoto ni muhandisi wa ujenzi wilaya ya ludewa Baraka Mkuya akiwa na Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya ludewa Edings Mwakambonja

 kundi la sanaa la IVA youth group lenye makao yake wilayani Ludewa likiburudisha siku ya familia
mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha akihutubia wananchi
Mwalimu Manongo wa shule ya msingi Ludewa kijijini akiselebuka na wanafunzi wake ngoma ya likwata



Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha ameapa kutowasaidia wananchi wilayani humo watakaokumbwa na balaa la njaa kutokana na wananchi hao kuanza kuvuna mahindi na kuyauza kwa bei rahisi na kusahau kuacha akiba ya baadae.


Bw.Madaha alisema takwimu inaonesha kwa mtu mzima moja ndani ya mwaka anatumia gunia tano za mahindi kwa chakula lakini baadhi ya wananchi huyauza mahindi yote kutokana na uroho wa fedha hali ambayo husababisha familia kuhangaika zinapokosa chakula na kuilaumu Serikali.


Alisema wilaya ya Ludewa kwa mwaka 2013 imeweza kupata mvua za kutosha kutona na hali hiyo hakuna kijiji wala kata ambacho kinaupungufu wa chakula itashangaza kama kuna familia zimeanza kuuza mazao na kutoacha akiba.


Aidha amewataka watendaji wa vijiji kulisimamia hilo na hatapokea taarifa yeyote ya kijiji wala kata itakayotaka chakula cha msaada kwa mwaka huu na mwaka ujao kutona na wilaya hiyo na wananchi wake kujitoshereza kwa chakula kama hakitatumiwa vibaya.


“Sitaomba chakula cha msaada kutoka Serikalini kwaajili ya kuwasaidia wananchi wa wilaya yangu ni bora nikafukuzwa kazi kwani mahindi yako yakutosha na anayeanza kuvuna na kuyauza kwa bei rahisi bila kuacha akiba shauli yake na serikali haitalaumiwa kwa hilo”alisema Bw.Madaha.

Bw.Madaha amewataka wakulima kuacha mara moja tabia ya kupokea fedha kwa wanunuzi wa mahindi kabla hayajavunwa kwani kuna wachuuzi hupita na kugawa fedha mapema ili waweze kujipatia mahindi hayo kwa bei rahisi msimu wa mavuno.


Nae Diwani wa kata ya Ludewa Bi.Monica Mchilo alisema imeshazoeleka kwa wananchi wa wilaya hiyo kuuza mazao yote na kushindwa hata chakula cha ziada hali inayosababisha serikali kulaumiwa kwa kutozisaidia baadhi ya kata zenye tabia hiyo.


Bi.Mchilo aliwataka wananchi wenye tabia kama hiyo kuacha mara moja kwani serikali iko kwaajili ya kusaidia maeneo ambayo mvua hazikunyesha na si maeneo kama Ludewa ambako mvua zimenyesha na mazao yamekubali lakini wananchi wanayauza bila ya kuacha akiba.


Alisema wilaya ya Ludewa ni kati ya wilaya nchini zenye rutuba yakutosha na inastawisha aina nyingi ya mazao hivyo itakuwa aibu kama Serikali itaombwa chakula cha msaada wakati kila kitu kinapatikana uzembe ni utunzaji tu.


“Tutatia aibu kwa taifa kama tutaomba chakula cha msaada wakati tuna kila kitu,ninacho waomba wananchi wenzangu ni kuacha tabia ya kuanza kupukucha mahindi na kuyauza mapema namna hii kwani thamani ya mahindi inapanda siku hadi siku tukiyatunza”alisema Bi.Mchilo.


Bi.Mchilo amewataka kunzia ngazi ya kaya kuanza kulindana kwa kukemea tabia ya kuza chakula chote bila ya kuacha akiba kutokana na hali halisi ya wilaya hiyo kupokea wageni wa migodini.


Mwisho.


No comments: