UGONJWA wa malaria na
mfumo wa hewa vimetajwa kuongoza kwa vifo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe
huku ushirikina na matumizi mabaya ya vyandarua vikitajwa kuwa vyanzo vikuu
vinavyosababisha kuongezeka kwa vifo hivyo.
Akizunguza jana
ofisini kwake mratibu wa maralia wilayani Ludewa Kelvin Mfuse alisema kundi
linaloongoza kwa vifo ni watoto wadogo chini ya miaka mitano na akina mama
wajawazito na wazee pamoja na waathrika wa virusi vya ukimwi ambao kinga zao za
mwili zimepungua.
’’’’ hali halisi ya
maambukizi ya malaria kiwilaya katika magonjwa kumi ambayo yalijitokeza kwa
wagonjwa wan je (OPD) malaria inaonekana inqonekana iko namba mbili ikianza ugonjwa
wa mfumo wa hewa.’’’’ Alisema Mfuse
Mfuse aliyataja
magonjwa hayo kuwa ni pamoja na Nimonia,kuharisha, upasuaji mdogo,magonjwa ya
ngozi, macho, ajali na magonjwa mengine, mfumo wa hewa na malaria inayoongoza
kwa vifo 59 kati ya vifo 158 ya vifo vilivyotokea kwenye vituo vya kutolea
hauduma sawa na asilimia 37 ya vifo kwa kipindi cha mwaka jana.
Aidha mratibu huyo alifafanua
kuwa wagonjwa 8248 walio chini ya miaka mitano kati ya wagonjwa 31,916
waliokuja kutibiwa walikuwa na malaria na wagonjwa wa malaria wenye umri zaidi
ya miaka mitano 13,608 walikuwa na malaria kati ya 41,394 sawa na asilimia 29 ya wagonjwa wote.
Dr Mfuse alizitaja
sababu zinazopelekea kupanda kwa vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria kuwa
ni pamoja na jamii kutokutumia vyandarua vilivyotolewa na serikali kwa
visingizio mbalimbali ikiwemo madai kuwa vyandarua hivyo hupunguza nguvu za
kiume.
Sababu zingine ni
wananchi kutumia vyandarua kwa matumizi yasiyorasmi kama vile kuvulia samaki
katika ziwa nyasa badala ya kutumia kuzuia mbu huku wengine wakitumia vyandarua
hivyo kufugia kuku majumbani.
Kauli mbiu ya siku ya
malaria mwaka huu wekeza kwa maisha yako ya baadaye kutokomeza malaria.
Hata hivyo kasi ndogo
ya kupambana na malaria katika wilaya ya Ludewa inasababishwa na changamoto kadhaa
ikiwemo jamii kukosa elimu juu ya matumizi sahihi ya vyandarua, ufinyu wa
bajeti kwa ajili ya kufikia malengo na uhaba wa watumishi hasa wale wenye sifa
za kitaaluma.
Wilaya ya Ludewa
imegawanyika katika kanda au maeneo makuu matatu ikiwemo ukanda wa juu sehemu
ya milimani ambako wanaamini hakuna malaria kutokana na hali ya hewa ya
ubaridi, sehemu ya ukanda wa kati ambao maambikizi yake ni wastani na ukanda wa
chini ambao maambukiza yake ni makubwa sababu ya kuwa na mazalia ya mengi ya
mbu.
mwisho
No comments:
Post a Comment