Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

May 04, 2013

ASKARI WACHANGA KUNUNUA UMEME KULIENDESHA GEREZA LUDEWA NA KUKARABATI NYUMBA KWA FEDHA BINAFSI.




        
ASKARI wa jeshi la magereza katika gereza la Ibihi lililoko wilaya Ludewa Mkoani Njombe wameamua kuchanga fedha kutoka katika mishahara yao ya kila mwezi ili kununua umeme wa Luku kusaidia kuliendesha gereza hilo kutokana na marereza mkoa kupeleka unit kidogo gerezani hapo imefahamika.

Wakizungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutoandikwa majina yao askari katika gereza hilo walisema wamekuwa wakitozwa jumla ya shilingi elfu kumi kila mmoja na kila mwezi ili kuweza kupata huduma hiyo muhimu ingawa wanapata umeme huo usiku tu. 

‘’’’’ tunashangazwa sana na serikali kushindwa kununua umeme wa kutosha kuendesha gereza hili usiku na mchana mpaka kupelekea askari kutozwa fedha kupitia mishahara na posho kwa ajili ya kuendeshea taasisi ya serikali.””” Walilalamika askari hao 

Wengine walikwenda mbali zaidi na kusema kuwa nyumba wanazoishi hazina hadhi ya kuishi binadamu au mtu mwenye familia kwa sababu siyo nyumba bali ni vibanda ambavyo hata hivyo kila askari hulazimika kufanya ukarabati mkubwa katika nyumba hizo ikiwa ni pamoja na kupiga sakafu kwa kutumia saruji ambapo hata akihama hawezi kurudishiwa.

Mkuu wa gereza hilo Charles Mbaga alikiri kuwepo kwa michango hiyo kutoka kwa askari kambini hapo na kwamba kila askari hulazimika kutoa mchnago wa jumla ya shilingi 10,000 kila mmoja ili kuendelelea kupata nishati hiyo muhimu.

Hata hivyo Mkuu huyo alikiri kupokea unit za miezi mitatu kama elfu tano kutoka kwa mkuu wa magereza mkoa wa Njombe lakini hazitoshi kumaliza mwezi hivyo pamoja na michango ya askari pamoja nay eye mwenyewe bado wanalazimika kuwasha umeme huo kuanzia saa 12 jioni.

‘’’’ mimi nilikotoka mbeya sijawahi kuona umeme ukikatika wala askari kuchangishwa hii ni ajabu lakini ndiyo ukweli wenyewe ulivyo taarifa kuhusu tatizo la umeme tumelifikisha ngazi za juu lakini uniti za umeme zinazokuja hazitoshi ndiyo maana tunalazimika kuchangia.’’’’ Aliongeza Mbaga

Naye mkuu wa magereza mkoa wa Iringa Kamishina mkuu msaidizi wa magereza Deusdedit Kamugisha akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alikataa kuwepo kwa taarifa za askari kuchangishwa na akasema kuwa amekuwa akituma fedha kwa ajili ya malipo ya umeme katika gereza hilo.

“” suala hili mimi silijui kwa sababu tanesco wamekuwa wakitishia kutukatia umeme kwa sababu hatujalipa bili sasa hilo suala la askari kuchangia fedha silijui lakini ninachotambua bili zinaletwa na tunalipa kupitia mfuko wa serikali kila siku wanaleta madeni na kila mwezi tunalipa.’’’’ Alisema Kamugisha

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ludewa ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Juma Madaha kwa upande wake alishangazwa na taarifa hiyo na kuahidi kulifuatilia suala hilo kwa kuzungumza na askari hao.

Kutokana na changamoto ya umeme gerezani hapo askari walilazimika kubuni mradi wa umeme wa maji lakini walishindwa kukamilisha kwa kukosa wataalam hata hivyo askari hao wamemwomba mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe kutoa msaada katika mradi huo.
                mwisho  

No comments: