Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

May 20, 2013

BABA MZAZI AJINYONGA BAADA YA MWANAE KUFA AKITOA MIMBA WILAYANI LUDEWA.





                Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP.Ngonyani

 Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Matema wilayani Ludewa mkoani Njombe amefariki Dunia Baada ya kushindikana kwa jaribio la kutoa mimba Nyumbani Kwa Mganga wa Zahanati ya Kijiji Cha Lifuma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Acp Fulgency Ngonyani amethibitisha kutokea kwa matukio hayo wilayani Ludewa.

Kamanda  Ngonyani amemtaja Binti huyo kuwa ni Grace Mwakila alieyefariki Dunia wakati akiwa nyumbani kwa mganga wa Zahanati hiyo wakati akijaribu kutoa mimba.

Amesema kuwa tukio hilo limetokea may 16 mwaka huu majira ya saa tisa alfajiri katika kijiji cha Lifuma ambapo mganga wa kituo cha afya Lifuma Dkt.Michael Nkoma alijaribu kumtoa mimba binti huyo na kumsababishia mauti.

Kamanda Ngonyani amesema kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi linamshikilia Mganga huyo aliyemtaja kwa jina la Michael Mkoma kwa mahojiano zaidi.
Taarifa zilizotufikia daktari huyo alipofanya jaribio la utoaji mimba na baada ya kushindwa na kumsababishia mauti manafunzi huyo alikaa na mwili wa mwanafunzi Grace ndani mwake kwa siku mbili ndipo alipoamua kutoa taarifa katika uongozi wa kijiji cha Lifuma kwa kuomba usalama wake.

 Baba mzazi wa binti aliyekufa kwa kutoa mimba Bw.Longinusi Mwakila amefariki dunia kwa kujinyonga na kamba ya Manila kufuatia kufariki kwa binti yake baada ya Kutoa Mimba.
Wananchi wa kijiji cha kilondo ambao hawakutaka majina yao yatajwe walisema kutokana na upendo wa Baba mzazi wa binti huyo kwa mwanae nae aliamua kujinyonga ili asishuhudie mazishi yamwanae aliyempenda.

Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya kujinyonga mkoani Njombe katika Kipindi cha mwezi mmoja na hivyo jeshi la Polisi kuwataka wananchi kutambua kuwa utoaji ni mimba ni kosa la Jinai ambalo ni hatari katika maisha Yao.
Hata hivyo baadhi ya ndugu wa marehemu hao wamelilalamikia jeshi la Polisi wilayani Ludewa kwa kutompeleka mtuhumiwa huyo mapema mahakani na kukaa nae kwa muda wa siku tano katika kituo cha polisi.
Mwisho

No comments: