Shirika
sililo la kiserikali la kiitaliano la ACRA linalofanya kazi wilayani Ludewa
katika mkoa wa Njombe jana limekutana na wadau mbalimbali wa elimu wilayani huo
ili kujua muhustakabali wa elimu na changamoto zake.
Warsha hiyo
iliyofanywa katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa iliwashirikisha
pia walimu waliowezeshwa na shirika hilo katika mafunzo mbalimbali ya elimu ya
msingi katika madarasa ya awali ilikujenga misingi bora ya elimu kuanzia ngazi
ya chini.
Akifungua
warsha hiyo ambayo ilikwenda sambamba na wiki ya elimu Duniani ambayo
huazimishwa kila mwaka Aprili 21 hadi 28 kwa mwaka 2013 ilikiwa na kauli mbiu
ya kila mtoto anahitaji mwalimu Afisa elimu wa wilaya ya Ludewa Robart Hyera
alisema walimu wanahitaji mafunzo ya mara kwa mara.
Bw.Hyera
alilisifu shirika la acra kwa kufanya mambo mengi katika elimu kwa wilaya ya
Ludewa yakiwemo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kata za
Mlangali,Mawengi na Milo pia kutoa mafunzo kwa walimu wa madarasa ya awali.
Alisema kumekuwa
na wimbi la walimu ambao tokea walipohitimu vyuoni hawajawahi kupata mafunzo
tena zaidi ya miaka kumi hali ambayo inazoofisha elimu za Tanzania na ndicho
chanzo kikuu cha kuzorota kwa elimu.
“Tumekuwa na
matatizo katika idara ya elimu kutokana na bajeti finyu ambayo imepelekea
kudorora kwa elimu kwani walimu walio wengi hawapati mafunzo ya mara kwa mara
ili kuboresha ujuzi wao jambo ambalo linasababisha matokeo mabovu kwa
wanafunzi”,alisema Bw.Hyera.
Meneja mradi
wa ACRA Bw.Beppe Buscaglia alisema shirika lake limefanya mambo mengi wilayani
Ludewa hasa katika ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu kutokana na shule
nyingine kuwa na vyumba vya madarasa vibovu.
Bw.Buscaglia
alisema matokeo ya shirika la acra kutoa mafunzo kwa walimu kupitia chuo cha
uwalimu cha Kreruu kumeleta ufanisi mkubwa ikiwa pamoja na ongezeko la ufaulu
na mahudhurio yawanafunzi.
Alisema
mpaka sasa jumla ya walimu wawili walipata mafunzo ambao ni mwalimu Tulamvona
Mturo miaka 52 wa shule ya msingi Mlangali ambaye anafundisha darasa la pili na
mwalimu Imelda Cassian Mtweve miaka 38 wa shule ya awali ulayasi ambaye
analipwa na jamii.
Aidha
mwalimu Imelda Mtweve anayefundisha madarasa ya awali katika shule ya msingi
Ulayasi alisema kabla ya kupata mafunzo alikuwa akiingia darasani na kuanza
kufundisha moja kwa moja bila ya kuwapa wanafunzi muda wa kucheza.
Alisema
wanafunzi walikuwa wanachoka mapema kutokana kutokujua mpangilio wa ufundishaji
hali ambayo ilipelekea wanafunzi karibia nusu ya darasa kutokujua kusoma na
kuandika pindi waingiapo darasa la kwanza.
Mwalimu
Imelda alisema kupitia mafunzo aliyoyapata kutoka shirika la acra ameweza
kuelewa saikolojia ya watoto na imekuwa rahisi kilimudu darasa kutokana na
kuzitambua tabia tofauti tofauti za wanafunzi anaowafundisha.
“Natumia
zana za kufundishia na kujifunzia pia nafurahia ufundishaji wangu wa sasa
kuliko zamani kwani awali sikujua jinsi ya kumudu na kupanga ufundishaji
wangu,nilitumia jitihada nyingi kufundisha lakini wanaojiunga darasa la kwanza
takribani nusu yao walikuwa hawajui kusoma na kuandika”,alisema mwalimu Imelda.
Nae Afisa
maendeleo ya jamii wa shirika la ACRA Bi.Neema Lazaro alisema licha ya ujenzi
na mafunzo yanayotolewa na shirika lake pia wanatoa viotabu vya masomo ya
hisabati na kiingereza katika shule za msingi za kata ya Milo,Mlangali na
Mawengi.
Bi.Neema
alisema pia baadhi ya madarasa ya awali katika kata hizo wametoa vifaa vya
kuchezea watoto na kuchora michoro katika kuta za madarasa hayo ambapo picha
hizo husaidia watoto kutambua vitu mbalimbali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment