Kikundi cha
sanaa chenye makao yake makuu wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kimepania
kuandaa Filamu itakayoonesha uhalisia wa mazingira ya wilaya hiyo kutokana na
vivutio vinavyopatikana ili kuitambulisha wilaya katika ulimwengu wa sanaa.
Hayo yalisemwa
jana na katibu wa IVA YOUTH GROUP Bi.Elizabeth Haule ambaye ni mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM (NEC) wakati wa mazoezi ya filamu hiyo katika ukumbi wa
ccm wilaya ya Ludewa.
Bi.Elizabeth
alisema kutokana na uhalisia na madhari nzuri ya wilaya ya Ludewa iliyopambwa
na milima yenye uoto wa asili,ziwa nyasa,machimbo ya dhahabu na makaa yam awe bila
kusahau chuma cha liganga filamu hiyo itakuwa ya kwanza kuonesha vivutio vya
asili.
Alisema
wilaya ya Ludewa ina wasanii wengi ambao bado hawajapata msukumo wa kuonesha
vipaji vyao hivyo ni fulsa pekee kwa wasanii hao kuungana na kufanya sanaa
itakayoitambulisha wilaya hiyo na vivutio vyake.
“Vijana
wengi wanapenda kuonesha uwezo wao katika sanaa mbalimbali lakini bado hawajapata
wadau wa kuwasaidia kuitangaza wilaya hii kwani inavivutio vingi ambavyo
havipatikani katika maeneo mengine nchini”,alisema Bi.Elizabeth.
Kundi hilo
limesajiriwa na Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) pia limeweza kufanya kazi za
uelimishaji hasa katika masuala ya afya kupitia mashirika mbalimbali lakini
bado halina mfadhiri ambaye ameweza kulisaidia kwa chochote zaidi ya wasanii
wenyewe kujichangisha ili kuendeleza sanaa zao.
Afisa
utamaduni wa wilaya ya Ludewa Bw.Shaban Bakari alisema yeye ndiye mwalimu pekee
aliyejitolea kwa wakati huu kulifundisha katika sanaa mbalimbali kutokana na
kutokuwa na mwalimu kwa kipindi kirefu.
Bw.Shaban
alisema vijana wengi wameweza kujiunga mpaka sasa jumla ya vijana 26 wamekuwa
wakihudhuria mazoezi ya Filamu hiyo na michezo mingine lakini bado wanakabiliwa
na changamoto nyingi.
Alisema
changamoto kubwa ya IVA YOUTH GROUP ni ukosefu wa vyombo vya sanaa kutokana na
wilaya hiyo kutokuwa na mwamko mkubwa wa makundi ya sanaa kwani hilo ni kundi
pekee ambalo limeweza kuonesha uhai.
Bw.Shabani
alisema baada ya kukamilisha mazoezi ya awali kundi hilo litafanya uzinduzi
rasmi wilayani humo ili kujitambulisha rasmi hivyo wadau mbalimbali wataalikwa
ili kutoa maoni yao yatakayoweza kuwaendeleza vijana hao katika tasnia ya
sanaa.
Aidha Suzan
Ng’ingo ambaye ni kaimu mwenyekiti wa IVA YOUTH GROUP aliwataka wasanii wa
kundi hilo kuwa wavumilivu kutokana na hali ngumu ya kifedha inayolikabili
kundi hilo.
Bi.Suzan uhalisia
wa filamu hiyo na mazingiora ya wilaya ya Ludewa ndio sifa pekee itakayoweza
kuwapatia heshima wasanii wa kundi hilo hasa kutokana na ukweli kwamba hakuna
kundi lolote la sanaa lililoweza rekodi filamu katika mazingira ya Ludewa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment