Wadau mbalimbali katika ukimbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakifuatilia maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa NJOCOBA
Mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Bw.Bazil Makungu akihojiana na afisa mikopo wa bank ya NJICOBA Bw.Danford Mfikwa
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Wiliam Waziri katika warsha hiyo ndani ya ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa
wadau wakitoa maoni yao jinsi ya ufanyaji kazi wa bank ya wananchi Njombe(NJOCOBA)
Kulia ni Mkurugenzi wa bank ya NJOCOBA Bw.Michael Ngwira akiwa na afisa ushirika wa mkoa wa Njombe Bw.Thomas Nyamba wakiandika maoni ya wadau.
Bank ya wananchi
Njombe(NJOCOBA)yenye makao yake mkuu mkoani Njombe imeamua kupanua huduma zake
kwa kufungua vituo vyake katika wilaya za Ludewa,Makete na mji wa Makambako ili
kuweza kuwafikishia huduma hiyo wateja wake.
Akizungumza jana wilayani
Ludewa Mkurugenzi mtendaji wa Bank hiyo Michael Ngwira aliitaka Halmashauri ya
wilaya ya Ludewa kutenga fedha kwa ajili ya kununua hisa katika benki hiyo ya
wananchi na kuwahamasisha watumishi na wananchi kununua hisa ili kukidhi vigezo
vya kufungua kituo cha kutolea huduma za kibenki.
Ngwira pamoja na
wataalamu wengine walitembelea wateja wa banki ya Njokoba katika wilaya ya
Ludewa wakiwa na lengo la kutoa ufafanuzi kuhusiana na masula ya mikopo na
manufaa ya saccos katika kupitia benki hiyo.
“”” benki ya Njocoba
ya mjini njombe ni mali ya wananchi wa wilaya zote za mkoa wa Njombe hivyo ni
fulsa pekee kwa wananchi hao kunufaika nayo kwa kupata mikopo midogo midogo
itakayowawezesha kufungua biashara za kuwasaidia kuondokana na umaskini.”””
Alisema Ngwira
Naye afisa mikopo wa
Njocoba Danford Mfikwa akawataka wateja wake kuwa na subira kwani vituo hivyo
vinatarajia kuanza rasmi juni mwaka huu ili kwenda sambamba na changamoto
zinazowakabili wananchi hasa wajasliamali wadogowadogo wasiokopesheka na
makampuni mengine nao waweze kukopa na kujiendesha kimaisha.
Bw.Mfikwa alisema
bank hiyo pia hutoa huduma za mikopo ya pembejeo kwa wateja wake pindi
wanapohitaji mikopo hiyo hivyo ni fulsa pekee kwa wateja wakulima kuchangamkia
mikopo hiyo.
Aliwataka wakulima wa
wilaya ya Ludewa na makete kujiunga na saccos mbalimbali ili waweze kukopesheka
kwani wakulima wa wilaya ya Njombe wameweza kunufaika na bank hiyo kupitia
vikundi vya kuweka na kukopa.
Nao washiriki wa
warsha hiyo wilayani Ludewa walifurahishwa na kuunga mkono jitihada za benki ya
Njocoba na kwamba wamechoshwa na usumbufu wa kutumia benki moja na kuomba
uongozi huo kufanya haraka kufungua tawi kwani wako tayari.
Katika ziara hiyo mkurugenzi wa njocoba
alifanikiwa kuzungumza na kikundi cha Rafiki ambacho kinataria kusajiriwa hivi
karibuni na kuwa mwanachama wa Njocoba.
Aidha Bw.Ngwira
aliwataka viongozi wa kikundi cha Rafiki kuutangazia umma ili wananchi wengi
waweze kujiunga na kikundi hicho kitakachoweza kupata mikopo kutoka bank
mbalimbali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment