Wadau wakichangia mawazo jinsi ya kuhifadhi mazingira wakati wa uanzishwaji migodi ya chuma na makaa ya mawe
wadau wakifuatilia kikao hicho
Prof Mwalyosi akielezea vipaumbele vya kuhifadhi mazingira katika miradi ya Mchuchuma na Liganga
Wakuu wa idara katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakifuatalia maelekezo katika kikao hi cho
Mkurugenzi wa Halmashsuri ya wilaya ya Ludewa Bw,William Waziri akitoa ufafanuzi jinsi wataalamu hao wa mazingira watakavyofanya kazi na wakuu wa idara mbalimbali wilayani Ludewa
Kulia Prof Mwalyosi na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakisikiliza michango ya wadau
wakuu wa idara mbalimbali wa halmashauri ya wilaya Ludewa wakifuatilia kikao hicho
Wataalamu wa mazingira kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam akichukua maoni ya wadauHayo yamesemwa jana na mbunge mstaafu wa jimbo la Ludewa Prof Raphael Mwalyosi katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo alipokutana na wakuu wa idara kuitambulisha timu ya wataalam wa mazingira waliofika kufanya utafiti kabla ya utekelezaji wa migodi ya Liganga na Mchuchuma ili kubaini athari na faida zitakazotokana na migodi hiyo.
“”” angalieni watu wa Ludewa mpaka sasa hawaamini kama migodi ya Liganga na Mchuchuma imeshaanza, maandalizi na matumizi ya fursa zitakazo tokana na migodi hiyo ni jukumu la wananchi wenyewe bila kutegemea wawekezaji.””” Alisema Mwalyosi
Mwalyosi aliongezakuwa katika kipindi chote cha uwakilishi wake alikuwa akiwataka wananchi washike ardhi la kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo hasa ile ya utoaji huduma kwa sababu siyo muda mrefu Ludewa itakuwa na ongezeko kubwa la watu watakao hitaji huduma za kibinadamu.
Katika kikao hicho wakuu wa Idara walibainisha mambo kadhaa yanayotakiwa kutekelezwa kabla machimbo kuanza ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji utakaojitokeza kutokana na migodi hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Wiliam Waziri aliwataka wakuu wa idara na wadau mbalimbali walioshiriki katika kikao hicho kuieleza jamii kuanza kuboresha maeneo mbalimbali ili kuwavutia wawekezaji.
Bw.Waziri alisema wananchi wa wilaya ya Ludewa kwa muda mrefu wamekuwa wakitaabika kutokana na hali ngumu ya maisha lakini kupitia miradi hiyo mikubwa wataweza kunufaika kwa kuuza mazao yao hali itakayowaongezea kipato.
Alisema kutokana na miradi hiyo kwenda haraka hata miundombinu itaboreshwa hivyo wilaya ya Ludewa itapata maendeleo haraka na kinachotakiwa kwa wananchi ni kumiliki ardhi na kutoiuza ovyo kwa wageni.
Aidha Prof Agnes Mwakaje aliwaomba wakuu wa idara kutoa ushiorikiano kwa watafiti wa mazingira ili kazi hiyo ya utafiti iweze kwenda haraka na kuwaruhusu wawekezaji kuanza kazi.
Prof.Mwakaje alisema kuwa wawekezaji wako tayari lakini kikubwa wanachokisubiri ni kupata kibari cha kuanza kazi na bila taarifa hiyo ya mazingira hawataweza kupata kibari hicho cha ufanyaji kazi.
Alisema Tanzania inapenda kuona wananchi wa maeneo husika wananufaika na miradi hiyo na si wananyanyasika na miradi inayowazunguka kutokana na hali hiyo ni lazima ufanyike utafiti wa mazingira ili kubaini athari na faida ya miradi hiyo.
“Haita pendeza kuona mambo yanayotokea Mtwara yakatokea Ludewa hivyo Serikali imeona ni vema kutuma wataalamu wa mazingira kabla miradi hiyo haijaanza,tunachokiomba kwa wananchi na wadau wengine ni ushirikiano ili tuwaishe taarifa hiyo”,alisema Prof Mwakaje.
Prof Mwakaje aliwataka wananchi wa Ludewa kujianda kikamili kwani inaonesha bado watu hawaamini kama miradi hiyo iko mbioni kuanza hivyo hata maandalizi ya kuandaa biashara kubwa na kilimo bora cha mazao ya chakula na matunda kinapaswa kunanza mapema ili kuwauzia wawekezaji na wafanyakazi wao.
TUNATOA HUDUMA ZETU KWA BEI RAHISI,PIA UNUNUAPO VIFAA VINGI UTAFIKISHIWA MPAKA NYUMBANI KWAKO.
KWA HUDUMA YA KUSUKA NJIA ZA UMEME WASILIANA NA MKURUGENZI WA NEW PWANI ELECTRICAL CONTRACTOR LUDEWA COMPANY SIM NO 026-2790004/0757-274594/0719239825
Kwa huduma za vifaa vya umeme huduma ya zima moto wilayani Ludewa wasiliana na NEW PWANI ELECTRICAL CONTRACTOR LUDEWA COMPANY kwa simu no 026-2790004/0757-274594/0719-239825 watakufikishia huduma hapo ulipo.
No comments:
Post a Comment