Wananchi wa
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe wametakiwa kuyapa ushirikiano mashirika
yasiyo ya kiserikali yanayokwenda kufanya kazi katika maeneo yao ili kuleta
maendeleo kwani kumekuwa na ugumu mkubwa kwa mashirika hayo katika utekelezaji
wa miradi vijijini.
Hayo
yamesemwa jana na mratibu wa miradi ya ujenzi wa shirika la ACRA kupitia mradi
wa INTERVITA Bi.Neema Kidugo wakati akikabidhi chumba cha darasa kilichojengwa
na shirika hilo kwa kushirikiana na wananchi katika shule ya msingi Mawengi.
Bi.Neema
alisema kumekuwa na ugumu mkubwa wa kazi katika baadhi ya vijiji wilayani
Ludewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali eidha kwa viongozi wa vijiji ama kwa
wananchi wenyewe hivyo wananchi wanapaswa kuelimishwa ili kushiriki kikamilifu
katika miradi inayotekelezwa katika vijiji vyao ili kuleta maendeleo zaidi
vijijini.
Shirika hilo
la ACRA kupitia mradi wa INTERVITA lenye
makao yake makuu nchini Italia limekuwa likijishughurisha na miradi mbalimbali
ya kijamii nchini ikiwemo miradi ya umeme vijijini,afya,maji,elimu na ujenzi wa
vyumba vya madarasa na vyoo salama.
Akisoma
taarifa ya ujenzi wa chumba hicho cha darasa Bi.Neema alisema ujenzi huo wa
darasa la shule ya msingi Mawengi umegharimu jumla ya shilingi million 19 na
laki 5 kati ya fedha hizo shilingi million 16 zilitolewa na shirika la ACRA
kupitia mradi wa INTERVITA na shilingi million 3.5 ni nguvu za wananchi
wenyewe.
“Jengo hilo
tulitakiwa tuwakabidhi Januari mwaka huu lakini kutokana na wananchi kuwa
nyumba katika shughuri mbalimbali za kimaendeleo tumeshindwa kulikabidhi kwa
wakati lakini bado tunaujenzi wa jengo jingine la darasa la awali hivyo
tunaomba wananchi watupatie ushirikiano wa kutosha sio sisi tu hata mashirika
mengine ili kukamilisha haraka miradi iaanyotekelezwa”,alisema Bi.Neema.
Bi.Neema
alisema ACRA wanakusudia kuendeleza ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika shule tano ambapo ujenzi huo utafanyika katika kata ya Mawengi,Milo na
Mlangali hivyo wananchi wa kata hizo wanatakiwa kijiandaa katika utekelezaji wa
miradi ya ujenzi kwa wakati.
Akikabidhiwa
jengo hilo la darasa Afisa elimu wa wilaya ya Ludewa Bw.Robart Hyera alilishukuru shirika la ACRA kupitia mradia
wa INTERVITA kutoka na shirika hilo kutekeleza miradi mingi na mikubwa katika
wilaya ya ludewa inayowanufaisha wananchi moja kwa moja.
Bw.Hyera
alisema ifike wakati wananchi waoneshe mchango wao kwa wafadhiri kama hao kwani
wamekuwa waiiunga mkono Serikali katika kufikisha maendeleo vijijini hivyo
hakuna sababu ya viongozi wa vijiji na wananchi kukwamisha miradi ya maendeleo
isitekelezwe.
Alisema
kumekuwa na changamoto nyingi katika shule za msingi wilayani Ludewa ikiwemo uhaba
wa vyumba vya madarasa lakini kupitia mashirika mbalimbali likiwemo shirika la
ACRA ukarabati na ujenzi wa madarasa umekuwa ukifanyika hivyo Serikali haina
budi kuyapongeza mashirika ya namna hiyo kutokana na juhudi yanayozifanya
katika kuboresha madarasa nchini.
Bw.Hyera
aliyataka mashirika mengine kuiga mfano wa shirika la ACRA katika kuhudumia
wananchi vijijini badala ya kujikita mjini ambako hakuna changamoto kubwa za
kimaisha kwani wananchi wa vijijini wakielimishwa wanaweza kutoa ushirikiano
katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Aidha meneja
mradi wa shirika la ACRA Bw.Beppe Buscaglia shirika hilo lilianza kufanya kazi
nchini mwaka 2006 katika jimbo katoriki la Njombe likitekeleza miradi ya umeme
na kuendeleza miradi ya ujenzi kupitia shirika la SHIPO kama mkandarasi katika
miradi ya ujenzi.
Shirika hilo
la ACRA limeanza kusambaza nishati ya umeme katika shule kumi ikiwa ni kata ya
Milo shule tano na kata ya Mawengi shule tano ili kuwawezesha wanafunzi wa
shule hizo kuweza kujisomea masomo ya jioni bila matatizo.
Naye fundi
mkuu msanifu wa shirika la SHIPO Bw.Vicent Mgina ambaye pia ni diwani wa kata
ya Mundindi alisema kupitia ACRA wamekuwa wakijenga na kutoa mafunzo kwa
mafundi ujenzi wa vijijini ili kuwawezeshz mafundi hao kwenda na wakati.
Bw.Mgina
alisema mafundi walioshiriki katika ujenzi wa jango la darasa la shule ya
msingi Mawengi wametunukiwa vyeti kutokana na kazi nzuri waliyoifanya hivyo
aliwasihi mafundi wa vijiji vingine ambako ujenzi utaendelea kujitokea ili
kunufaika na mafunzo yatakayotolewa na SHIPO.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment