Mwenyekiti
wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Matei Felisian Kongo jana alisinda kesi
iliyokuwa ikimkabili ya kuomba na kupokea rushwa kwa Bw.Solomon Mwaikugile
machi 14,mwaka 2012 na kuachiwa huru katika mahaka ya wilaya ya Ludewa.
Akisoma
hukumu hiyo katika mahaka ya wilaya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Ludewa
Mh.Frederik Lukuna alisema sababu ya kwanza iliyomfanya mshtakiwa aachiwe huru
ilikuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha kwa maandishi kuwa Bw.Matei
Kongo alikuwa anakesi ya kujibu.
Mh.Lukuna
alisema sababu ya pili ilikuwa shahidi namba moja ambaye ni Bw.Solomon
Mwaikugile alimtafuta Bw.Kongo ili amshawishi na si kongo aliyemshawishi Bw.Mwaikugile.
Sababu ya
tatu ilikuwa ni kampuni ya Bw.Mwaikugile haikuomba tenda na hakuna sehemu
inayoonesha Bw.Kongo aliomba rushwa ya shilingi million tatu,pia alipewa fedha
ya mafuta kupitia katika account ya Aidan Luoga katika bank ya NMB tawi la
Ludewa na kabla hajapata fedha hiyo tayari mwenye ambako fedha ilipitia akakamatwa.
Bw.Mwaikugile
aliithibitishia Mahakama kuwa aliitoa shilingi laki moja kama fedha ya mafuta
ya pikipiki kwaajili ya kumtoa Bw.Kongo kutoka Luilo hadi Ludewa Mjini ili
kusafisha njia ya kupata zabuni.
Mh.Hakimu
alisema kutokana na ushahidi wa mtoaji fedha haioneshi kama Bw.Kongo aliiomba
fedha hiyo zaidi ya Bw.Mwaikugile kumshawishi ili aweze kuunganisha na wajumbe
wa bodi ya zabuni ili afanikiwe mambo yake.
Mh.Lukuna
alisema kwa upande wa mwenyekiti wa wilaya ya Ludewa wa bodi ya zabuni
Bw.Lazaro Mapunda alikiri mbele ya mahakama kuwa Bw.Kongo hakuwa mjumbe wa bodi
hiyo hivyo alikuwa hana uwezo wa kumpatia uzabuni mkandarasi.
Alisema kesi
hiyo imesikilizwa upande wa mashtaka pekee na jumla ya mashahidi nane walitoa
ushahidiambapo kupitia sheria katika kifungu 15 A na B ya kuomba na kupokea
rushwa ya kuzuia na kupambana na rushwa sheria namba 11 ya mwaka 2007 ndiyo
iliyoamuru Bw.Kongo kuachiwa huru.
“kutokana na
vielelezo zilivyotoleawa pamoja na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na
kushindwa kuthibitisha kama Bw.Kongo anakesi ya kujibu na kupitia vifungu vya
sheria ya kuomba na kupokea rushwa mahakama inamuachia huru kwakua hana kesi ya
kujibu”,alisema Mh.Lukuna.
Awali ilidaiwa
mahakamani hapo kuwa kati ya oktoba mwaka jana na machi mwaka huu mshtakiwa
Matei Kongo aliomba rushwa kwa Samson
Mwaipugile mkazi wa Dar es Salaam ili aweze kumpa kwa upendeleo tenda ya ujenzi
wa barabara na kusambaza vifaa vya ofisi ikiwemo komputa katika halmashauri ya
wilaya ya Ludewa.
Mwenyekiti huyo wa
halmashauri ya wilaya ya Ludewa alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa madai
kuwa machi 12 mwaka huu alipokea rushwa ya shilingi laki moja (100,000) kwanjia
ya benki ya NMB Tawi la Ludewa kupitia
akaunti ya Aidan Luoga.
Katika hali
iliyowashangaza wasikilizaji shahidi wa mwisho katika kesi hiyo ambaye anatajwa
kuwa rafiki mkubwa wa mshtakiwa Bw Aidani Luoga akaiambia mahakama kuwa machi
12 mwaka huu mshtakiwa alikwenda kwake kuomba namba ya akaunti ya NMB akampa
lakini akashangaa siku hiyo majira ya saa 9 mchana akakamatwa na takukuru.
Kwa upande wa
mashtaka yaani taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)kesi hiyo
ilisimamiwa na mwanasheria msomi Bi. Restuta Kessy na kwa upande wa mshtakiwa ilisimamiwa na
wakili wa kujitegemea Bw. Frank Ngafumika mpaka
ilipofikia tamati.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment