Mtoto Juliana akiwa katika hali ya kuridhisha baada ya matibabu
Huyu ndio Bi.Jemidah Kulanga aliye mtafutia mfadhiri mtoto Juliana hapo akiwa na mtoto huyo katika Hospitari ya Taifa ya Muhimbili
Kushoto ni Bw.Katambala akisaidiana na bibi wa mtoto Juliana wakimnywesha uji hospitari ya CCBRT
Katikati Mtoto Juliana Mwinuka kulia ni Bw.Katambala na kushoto ni Bi.Magreth Mahanje wakiwa katika gari ya mfadhiri Bi.Mariam wakielekea katika Hospitari ya Taifa ya Muhimbili.
Kushoto Bi.Jemida Kulangaakuhudhuria kikao ndipo alipo pata picha ya Mtoto Juliana Mwinuka na kumuunganisha kwa Mfadhiri.
Mtoto Juliana baada ya Matibabu
Mtoto Juliana Mwinuka kabla ya matibabu
Tunaomba radhi kwa picha hizi.
Shirika lisilo
la Kiserikali la MISO(Milo Sayuni Ophans) Lenye makao yake makuu wilayani
Ludewa katika mkoa wa Njombe linatoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali
walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika michango yao iliyomwezesha mtoto
Juliana Mwinuka aliyeungua moto kwaajili ya matibabu.
Akiongea na
waandishi wa habari leo Afisa tathmini na ufuatiliaji wa shirika la MISO
Bw.Geofrey Katambala alisema shirika hilo kupitia mradi wa Africare waliweza
kumuibua mtoto huyo katika kijiji cha Mbugani kata ya Mavanga wilayani Ludewa
na kutafuta wadhiri walioweza kumsaidia.
Alisema
haikuwa kazi rahisi kumpata mfadhiri lakini kutokana na nguvu za Bi.Jemida Kulanga
aliweza kuliunganisha shirika hilo na wakinadada wawili ambao ni Bi.Mariam
Masawe na Halima Mohammed lakini safari ya ufadhiri wa Juliana pale ambapo
mmjoa wa wafadhiri hao Bi.Halima Mohammed kufariki dunia kwa ajari ya gari.
Bw.Katambala
alisema alibaki mfadhiri mmoja ambaye ni Bi.Mariam ambaye aliendelea kutoa
msaada kuanzia mtoto huyo alipo fikishwa katika hospitari ya Taifa ya Muhimbili
na baadae kuhamishiwa katika hospitari ya CCBRT kwaajili ya kuwekewa ngozi nyingine
usoni kutokana na uso wa mtoto huyo kuteketea kwa moto.
“Tunawashukuru
wadau mbalimbali kutokana na misaada yao ya hali na mali hasa Bi.Mariam
Masawe,Bi.Jemida Kulanga na mwanahabari Francis Godwin kupitia mtandao wake
kwani wadau waliweza kuziona picha za mtoto huyo na kuguswa na jambo hilo”,alisema
Bw.Katambala.
Alisema
mpaka sasa mtoto huyo ameweza kutibiwa vizuri na kurudishiwa ngozi ya uso wake
na yupo kijijini kwake na anaendelea vizuri akihudumiwa na bibi yake Magreth
Mahanje wakiendelea na kilimo cha zao la mahindi.
Aidha
Bw.Katambala aliwataka wadau kuendelea kumchangia mtoto huyo kwa bado
anahitajika kurudi hospitari baada ya miezi mitatu ili kuendelea kufanyiwa
upasuaji na ubandikaji wa ngozi maeneo mengine hasa maeneo ya jicho lake la kulia.
Alisema
jicho la kushoto liko sawa lakini jicho la kulia bado lina matatizo hivyo
madaktari walishauri kuwa ataendelaa kupata matibabu ili aweze kurudi katika
hali yake kwani bado ana umri mdogo anaweza kufanya shughuri za uzalishaji
baadae.
Hata hivyo
shirika la miso linampango wa kumuanzisha shule ili apate elimu itakayo weza
kumsaidia katika maisha yake kwani anauwezo mzuri akipata msaada wa kuendelezwa
kielimu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment