Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 30, 2013

JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LASISITIZA AMANI SIKUKUU YA PASAKA







                               Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani
Wakati Waumini wa Dini ya Kikristo Duniani Kote Hapo Kesho Wakitarajia Kusherehekea Sikukuu ya Pasaka Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limesema Limejipanga Kuimarisha Ulinzi na Usalama Katika Kipindi Hiki Cha Sikukuu Hizo  na Hivyo Kuwataka Wananchi Kusherehekea Sikukuu Hizo na Kuendelea na Ibada Bila Wasiwasi Wowote.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi Fulgency Ngonyani Amesema Katika Kipindi Chote Cha Sikukuu Jeshi Hilo Litakuwa Likiendelea na Oparesheni Katika Mitaa Mbalimabali Huku Wakitoa Wito Kwa Wamiliki wa Kumbi za Burudani Kuzingatia Usalama wa Wananchi.

Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Amewatakia Kheri ya Pasaka Wananchi Wote na Waumini wa Dini ya Kikristo na Kuwataka Kusherehekea Sikukuu Hiyo Kwa Amani na Utulivu.

Wakati Huo Huo Waumini wa Makanisa ya Kikristo Wameaswa Kuachana na Matendo Maovu na Badala Yake Wamrudie Mungu na Kufufuka Pamoja na Kristo.

Akiongea na Waumini wa Kanisa Katoliki Katika Mafundisho ya Ijumaa Kuu Paroko Msaidizi wa Parokia ya Njombe Padre Fortunatus Mwinuka Amesema Wakristo Wanapaswa Kufuata Misingi ya Dini Yao na Kuhakikisha Wanabadili Matendo Yao kwa Kuwasaidia Wale Wasiojiweza,Wagonjwa Yatima,na Walemavu.

 Na Gabriel Kilamlya,Njombe.



No comments: