Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 30, 2013

BARABARA YA MAKETE,MBEYA YAWA KATIKA HALI MBAYA






Mkuu wa wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro amewataka wananchi  wa makete  kushiriki katika  ukarabati wa miundombinu ya barabara pindi tatizo linapotokea hasa maeneo korofi

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu kwa njia ya simu Bi.Matiro alisema wananchi wanatakiwa kuwa na ushirikiano pindi barabara zinapokuwa zimeharibika ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Makete

Hata hivyo alisema kuwa viongozi wa Tanrods ameshapewa taarifa kuhusiana na tatizo hilo lililoko ktk maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo hasa katika kijiji cha Ivalalila ambapo magari ya kutoka Mbeya kuja makete yanashindwa kupita kulingana na ubovu wa barabara hiyo

Mtandao huu ulifika eneo la tukio nakujionea hali halisi  ya barabara ambapo mpaka sasa hakuna mawasiliano kutoka Makete kwenda jijini mbeya kutokana na shimo lililopo eneo la Ivalalila.
 
 Mtandao huu haukiishia hapo ulikwenda moja kwa moja kuongea na wamiliki wa vyombo vya usari ambapo mmiliki wa kampuni ya Japanice Junich Daniel alimarufu kama  Mwarabu alisema "kwa hali hii inakoelekea usafiri wa Makete na Mbeya hautakuwepo kutokana na tunaingia gharama nyingi kufanya marekebisho ya magari kutokana na mara nyingi kugongesha katika mashimo ya barabarani"

Akiendelea Mwarabu alisema"natumia fursa hii kumuomba mbuge na uongozi mzima bila kumsahau waziri mwenye dhamana kuweza kutufanyia marekebisho katika barabara za wilaya ya makete kuwa hali tete hususani nyakati za masika 

Na Riziki Mgaya,Makete


No comments: