Jengo mojawapo la shule ya Msingi Amani lililoezuliwa kwa Mvua zilizoambatana na upepo
Wanafunzi wa shule ya msingi Amani wakiwa nje ya shule yao iliyoezuliwa kwa mvua
Baadhi ya majengo ya shule ya msingi Amani yaliyoezuliwa na mvua
Mjengo ya Shule ya Msingi Amani yakiwa katika hali mbaya baada ya kuezuliwa na Mvua zilizoambatana na upepo
Bati za shule hiyo zikiwa zimetupwa juu ya miti na mvua zilizoambatana na upepo.
Maafa makubwa yameikumba shule ya msingi Amani iliyoko kijiji cha Amani kata ya Mundindi baada ya shule hiyo kuezuliwa paa zake kwa upepo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea wilayani Ludewa kwa msimu huu wa masika.
Akizungumza na mtandao huu Diwani wa kata ya Mundindi Bw.Vincent Mgina alisema shule hiyo ambayo ni kongwe kwa kijiji cha Amani ilikubwa na mkasa huo hivi karibuni ambapo hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa kutokana na maafa hayo.
Mh.Mgina alisema juhudi zakuilejesha shule hiyo katika hali yake ya mwanzo ili wanafunzi waendelee na masomo zinaendelea kufanyika ambapo ameshakutana na uongozi wa wilaya ya Ludewa na mkurugenzzi wa wilaya hiyo Bw.Fidelis Lumato kuzungumzia sakata hilo.
Alisema uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kupitia kamati ya maafa umeliona hilo na inalifanyia kazi lakini tayali imeundwa kamati ya kijiji inayoendelea kulishughurikia suala hilo kwa kupitia michango ya wananchi ili kuyanusuru majengo ya shule hiyo yasiendelee kuharibiwa na mvua.
Aidha Mh.Mgina alisema wananchi pekee hawawezi kuchangisha michango na kufanikisha ukarabati wa majengo hayo hivyo anaiomba Serikali kupitia kitengo cha maafa kuharakisha ukarabati wa shule hiyo ili wanafunzi waendelee na masomo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment