Wakwanza kushoto ni katibu wa NJOREFA Bw.Njowoka,katikati ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha na mwenye kijani ni katibu wa LUDIFA Bw.Mvanginyi
Katibu wa NJOREFA Bw.Njowoka akimkabidhi mkuuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha sale za waamuzi
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akitoa hotuba baada ya kukabidhiwa vifaa vya waamuzi leo katika viwanja vya leaders Ludewa mjini
Katubu wa NJOREFA Bw.Njowoka akitoa maelezo kuhusiana na upatikanaji wa vifaa hivyo
Wadau mbalimbali wa soka wakimsikiliza Bw.Njowoka katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya waamuzi
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akimshukuru Bw.Njowoka kwa ufadhiri wa vifaa vya waamuzi wilaya ya Ludewa
Hivi ni baadhi ya vifaa vya waaamuzi alivyovitoa Bw.Njowoka leo wilayani Ludewa
Katibu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Ludewa Bw.Mvanginyi akishukuru baada ya kupata vifaa hivyo
Mmoja wa waamuzi wa mpambano wa leo kati ya timu ya kurugenzi Ludewa na National ya Lugarawa katika ligi daraja la pili ,timu zote zikiwa zinatoka ndani ya wilaya ya Ludewa
Waamuzi kutoka njombe wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni kiongozi wa timu ya Kurugenzi Ludewa Bw.Agrey Mwinuka na katibu wa NJOREFA Bw.Njowoka
Katibu wa NJOREFA Bw.Njowoka akitoa maelezo ya ufadhiri wake kutokana na upatikanaji wa vifaa hivyo ulivyofanyika
Chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Ludewa(LUDIFA) kimepata
ufadhiri wa vifaa vya Waamuzi kutoka kwa wadau wa soka kutokana na waamuzi
wilayani humo kwa miaka mingi kutokuwa na vifaa zikiwemo sale za kuendeshea
mashindano mbalimbali yanayoendelea.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Katibu wa
chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Njombe(NJOREFA) Bw.Steven Njowoka alisema kuwa
kutokana na muonekano wa soka katika wilaya ya Ludewa si Vema waamuzi
wakaendesha mashindano bila vifaa vya kisasa.
Bw.Njowoka alisema yeye aliona umuhimu wa Waamuzi kuwa na
vifaa vya kisasa katika kuliendeleza soka na kama mzawa wa wilaya ya Ludewa
akaamua kukutana na wadau mbalimbali ili kuweza kuwasaidia waamuzi hao katika
vifaa vya muhimu.
Alisema wafadhiri waliojitokeza kuwa saidia waamuzi hao ni
Bw.Kasian Njowoka ambaye ni mmiliki wa chuo cha uwalimu Kibamba(Kibamba
Teachers College)amesaidia sale pea nne,Filimbi,Kadi na pendera za waamuzi
wasaidizi,mwingine ni Bw.Stanley Lugenge ambaye ni mwenyekiti wa chama cha
mpira wa miguu Njombe katoa sale za waamuzi pea nne.
Bw.Njowoka alisema yeye aliamua kutoa msaada waNyavu za
magoli na mpira mmoja vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki mbili na
nusu(250000)kwa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Ludewa(LUDIFA) ili kuona
mashindano ya ligi daraja la pili yanayoendelea mkoa wa Njombe yanaendeshwa
ipasavyo.
“Nimeona umuhimu wa kuendeleza soka mkoa wa Njombe hususani
wilaya ya Ludewa kutokana na muda mrefu waamuzi kutokuwa na vifaa hivyo mimi
nikaamua kuwaona wadau wanaoweza kuniunga mkono kuwasaidia waamuzi hawa hivyo
huu ni mwanzo tu tutaendelea kutoa vifaa vingine”,alisema Bw.Njowoka.
Awali waamuzi wa mpira wa miguu walikuwa wakivaa suti na
mavazi mengine yasiyo ya kimishezo katika kuhakikisha soka wilayani Ludewa
linaendelea hivyo kwa vifaa hivi wataweza kuchezesha kwa uhuru hasa pale
inapobidi kukimbia na kutoa maamuzi ya haraka.
Bw.Njowoka alisema mmiliki wa chuo cha uwalimu Kibamba
Bw.Kasian Njowoka aliahidi kuendelea kukisaidia chama cha mpira wa miguu wilaya
ya Ludewa kutokana na chama hicho kutokuwa na vifaa vya michezo tangia
kianzishwe.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha
akikabidhiwa vifaa hivyo aliwapongeza wadau wa soka waliojitokeza kukisaidia
chama cha mpira wa miguu wilaya ya Ludewa na kuwataka waendelee na moyo huo
kwani michezo hujenga undugu.
Bw.Madaha alisema amefurahishwa na msaada huo kwani katika
mashindano ya ligi daraja la pili yanayoendelea mkoa wa njombe yanayozishirikisha
timu nne za wilaya wilaya ya Ludewa ni haibu kuona waamunzi wa wilaya hiyo
wakichezesha mashindano hayo bila kuwa na sale maalumu.
Alisema ofisi yake itaongeza sale nyingine kwani hata
walizoleta wafadhiri hao bado ni chache hiyo ni changamoto ya wilaya kuwa na
sale zaidi kutokana na ugumu wa kazi ya uamuzi ambapo bila kuwa na vifaa vya
kutosha ugumu wa kazi hiyo utazidi.
Bw.Madaha alisema yeye kama mdau wa soka yuko bega kwa began
a chama cha mpira wa miguu wilaya ya Ludewa kwani anaandaa mkutano na wadau
mbalimbali wakiwemo wawekezaji walioko katika wilaya hiyo ili kuona namna ya
kuuwezesha mchezo huo kusonga mbele.
Nae katibu wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Ludewa
(LUDIFA)Bw.Mvanginyi akishukuru baada ya kupata vifaa hivyo alisema chama chao
kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za ukosefu wa fedha za kujiendesha
hivyo anawashukuru wafadhiri kwa kutoa msaada huo.
Bw.Mvanginyi alisema Mkuu wa wilaya ya Ludewa ni mdau mkubwa
wa soka hivyo anaiomba serikali kupitia mkuu huyo kukamilisha haraka ujenzi wa
uwanja unaoendelea ili chama hicho kiweze kujipatia mapato yatakayoweza kutatua
mahitaji madogomadogo ya chama hicho.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment