Wafuasi wa CCM akimpiga kwa mawe kada wa CHADEMA
Ragge akigombea mtu wa bendela na mfuasi wa CHADEMA
Wafuasi wa CCM wakigombaniana mti wa Bendela na wafuasi wa Chadema
Ragge na wafuasi wengine wa CCM wakipambana na mfuasi wa CHADEMA
Kada wa CHADEMA Idd Kizito akidhibitiwa na Polisi
SHEREHE
za miaka 36 za kuzaliwa kwa CCM jana ziliingia dosari, baada ya kuibuka vurugu
kubwa kati ya wafuasi wa chama hicho na Chadema mkoani Dodoma wakati wakigombea
eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.
Kada
wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akikimbizwa na wafuasi wa CCM jana, baada
ya kutokea vurugu katika eneo la Mwanga baa, Dodoma
Vurugu
hizo zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana mchana
katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM kung’oa bendera
ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera zao kwa ajili ya
mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho hayo.
Vurugu
zilizuka baada ya wafuasi wa Chadema kuwataka wenzao wa CCM waendelee na
mkutano katika eneo hilo kwa sharti la kurejeshwa kwa bendera iliyong’olewa.
Wafuasi wa vyama hivyo wakiwamo wabunge wa CCM walionekana wakivutana
kunyang’anyana mti wa bendera.
“Baada ya CCM kugoma, Chadema walijaribu kurudisha bendera hiyo kwa
nguvu, jambo ambalo lilifanya wafuasi wa CCM waanze kuokota mawe na kuwarushia
wapinzani wao hao, huku Chadema nao walianza kujibu mapigo,” alisema mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo.
Baadhi
ya wabunge wa CCM walioshiriki katika vurugu hizo na majimbo yao kwenye mabano
ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Nyambari Nyangwine (Tarime), Seleman Jafo
(Kisarawe), Said Mtanda (Mchinga) na Mary Chatanda (Viti Maalumu).
Baadhi
ya wafuasi wa CCM walionekana wakibeba mawe na kuwapiga wenzao wa Chadema na
kusababisha tafrani kubwa katika eneo hilo la mkutano.
Katibu
wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Jellah Mambo alisema kuwa tukio hilo
limetokana na wafuasi wa CCM kung’oa bendera ya Chadema iliyokuwa ikipepea eneo
la Mwanga Baa kulikofanyika sherehe za chama chao (CCM).
“Kwanza wamechukua bendera yetu. Halafu tumeshangazwa na CCM
kuruhusiwa kufanya maadhimisho yao wakati kuna agizo la Mkuu wa Mkoa na polisi
kukataza mikusanyiko ya kisiasa wakati wa Bunge.
“Kwa nini sisi (Chadema) tuzuiwe mikutano yetu wakati wenzetu
wanafanya? Huku si kutenda haki....Tulikuwa na mikutano ya kuimarisha chama
katika kata kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, lakini tumezuiwa na
tukaheshimu mamlaka,”
alisema katibu huyo.
Pia
tulikuwa tufanye mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, lakini
tukazuiwa na tuliheshimu amri hiyo, alisema.
Mambo
alisema katika vurugu hizo wafuasi wawili wa Chadema; Idd Kizota na Anord Swai
waliumizwa na kushonwa nyuzi saba usoni.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya alisema hana taarifa za
majeruhi hao.
No comments:
Post a Comment