Askari wa kikosi cha kuzima moto akiuzima moto ulioshika katika maduka hayo
vikosi vya usalama vikiwa kazini eneo la maduka ya vipodozi Mwenge Jijini Dar es Salaam
wafanya biashara wkijaribu kuokoa mali zao zilizosalia
mashuhuda wa tukio hilo akiangalia zoezi la uzimaji moto linavyoendelea
vikosi vya usalama vikiangalia usalama wa eneo hilo
Mduka yakiwa yameshika moto eneo la mwenge
MADUKA kadhaa ya vipodozi, nguo yameungua moto na
kusababisha hasara kubwa kwa wamiliki wake.
Moto huo umetokea mishale ya saa 5.20 leo asubuhi baada ya kutokea hitilafu ya umeme kwenye moja ya kibanda cha biashara.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, moto huo ulianza taratibu kisha kupamba moto.
Wafanyabiashara wa maduka ya vipodozi ndiyo waliopata hasara kubwa kwa mali zao kuharibika kufuatia kutaka kuziokoa.
Hata hivyo, Kikosi cha Zima moto kilichofika eneo la tukio kwa wakati na kimepongezwa kwa kufanya kazi nzuri na kuweza kuudhibiti moto huo.
Adha, jeshi la polisi limepongezwa kwa kazi nzuri lililoifanya ya kudhibiti vibaka ambao walijiandaa kufanya uhalifu wa kuiba mali katika kurupushani hizo za uokoaji.

No comments:
Post a Comment