February 01, 2013
HALMASHAURI YA WILAYA LUDEWA YAPITISHA MAKADILIO YA BAJETI YA MWAKA 2013/2014
Mkutano wa baraza la Madiwani katika Halmashauri ya wilaya Ludewa wa kujadili mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2013/2014 umefanyika leo ambapo makisio ya bajeti hiyo yanakadiliwa kufikia zaidi ya kiasi cha shilingi 150 bilioni.
Akisoma bajeti hiyo katika kikao cha baraza la madiwani mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Ludewa Bw.Fidelis Lumato alisema bajeti hiyo inatokana na mapato ya ndani ambayo halmashauri inakadiria kuyakusana na fedha za ruzuku kutoka Hazina.
Alisema mapendekezo ya bajeti hiyo yalikuwa yakisubiri Baraka za baraza la madiwani ndipo yafikishwe mahara husika hivyo aliwataka madiwani kuwa watulivu mpaka bajeti hiyo itakapo idhinishwa makao makuu.
Bw.Lumato alisema katika bajeti hiyo pia kuna mapendekezo ya maombi maalum nje ya ukomo wa bajeti kwa mwaka 2013/2014 ambayo inafikia shilingi billion 1.5 ambayo imelenga katika ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti,ujenzi wa boma,ujenzi wa maabara na hostel.
“mapendekezo ya maombi maalumu nje ya bajeti ndicho kilichokuwa kinaniumiza kichwa maana imelenga maeneo muhimu ambayo ni kero kwa wilaya ya Ludewa hivyo ni matarajio yetu ikishapitishwa hazina utakuwa ni ukombozi kwetu”,alisema Bw.Lumato.
Aidha mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni diwani wa kata ya Luilo Bw.Matei Kongo aliwataka madiwani kusimamia miradi iliyobuniwa na wataalamu na kuiandalia bajeti ambayo ndio iliyopitishwa na baraza hilo.
Bw.Kongo alisema kumekuwa na usimamizi mbovu wa fedha za maendeleo pindi zinapotolewa toka hazina kutokana na madiwani walio wengi kutojihusisha na usimamizi wa fedha hizo badala yake madiwani hao husubiri kuwalaumu wataalamu kwenye vikao badala ya kuwasaidia.
Alisema katika mapendekezo ya bajeti hii kama itapitishwa na hazina basi diwani wa kata husika ndiye atakeyepaswa kutoa taarifa ya miradi inayotekelezwa katika kata yake na mchanganuo wa matumizi ya fedha katika miradi hiyo.
Bw.Kongo aliwataka madiwani wenzake kuacha tabia ya kushabikia vyama na badala yake kuchapa kazi kwani ndicho walichotumwa na wananchi na masuala vya vyama vya siasa huishia katika chaguzi na si katika vikao vya utendaji.
Nae mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha aliwataka madiwani hao kuwa wakati wanapoona miradi ya maendeleo inasuasua wakati fedha za miradi hiyo zimetolewa na Serikali.
Alisema ili kuleta ufanisi katika bajeti mbalimbali zinazoandaliwa na Serikali ni usimamizi mzuri na kuwakemea watendaji wanaoonesha kutokuwa waaminifu katika kutekeleza miradi hiyo.
Bw.Madaha alisema kupitia mapendekezo ya bajeti hiyo madiwani wanapaswa kuwaelimisha wananchi kujiunga na Vikoba,Sacos na vyama vya ushirika ili kuweza kujipatia mikopo na pembejeo kuanzia mwakani.
Alisema yawezekana kuanzia mwaka 2014 Serikali itawapatia wakulima ruzuku ya pembejeo kwa kupitia vyama hivyo kwani mdhamini mkuu ili mwananchi upate pembejeo atakuwa ni kikundi ulichojiunga.
Bw.Madaha aliwataka Madiwani kuwa chachu ya maendeleo katika kata zao ambapo watatakiwa kuwahimiza watendaji katika ukusanyaji mapato ya ndani ili wilaya iweze kijiendesha bila ya ukata wa fedha uliokithiri kwa sasa.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment