Na Nickson Mahundi ,Njombe.
Kwa siku ya tatu sasa mji wa njombe umekumbwa na adha ya
kukosekana kwa nishati ya mafuta ya petrol kwenye vituo vya mafuta hali
inayopelekea kukwama kwa usafiri na kushuka kwa uchumi miongoni mwa jamii.
Hali hiyo ilitokea septemba 30 mwezi uliopita hadi sasa
ambapo hadi hii leo ni kituo kimoja cha ndime petrolstation pekee ndicho
kilichofanikiwa kuleta aina hiyo ya mafuta.
Wakizungumza na mwandishi wetu jana kwa nyakati tofauti
baadhi ya madereva wa magari na pikipiki mjini njombe wamesema kuwa adha hiyo
imepelekea baadhi ya magari na pikipiki kuzima njiani yakiwa na abiria kitu
ambacho kimeleta usumbufu kwa abiria.
Meneja wa kituo
cha ndime petrolstation,Bw.Prosper
Mtewele na kaimu meneja wa kituo cha mafuta total walisema tatizo hilo limetokana
na kituo kikubwa cha kusambaza mafuta kutofanya kazi hiyo kwa siku za jumamosi
na jumapili.
Kutokana na hali hiyo ndio sababau kubwa ya kukosekana kwa
nishati hiyo ambayo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wahitaji kwa wamekuwa
wakitumia muda mrefu katika foreni ya kupata nishati hiyo.
“kutokana na wasambazaji wakuu kutofanya kazi siku za
jumamosi na jumapili imepelekea tatizo hili lakini wanashindwa kutambua huu
sasa ni mkoa na si kama ilivyokuwa awali,tunapata usumbufu mkubwa kwa wateja”,alisema
meneja Mtewele.
Hat hivyo pamoja na kutokuwepo kwa mafuta mjini njombe
hakuna ongezeko lolote la bei ya mafuta lililo ongezeka mkoani hapa.
Aidha madereva wamekerwa na kulazimika kununua mafuta katika
wilaya na mikoa ya jirani wawapo safarini ili kuepuka usumbufu wanaoupata
Njombe.
MWISHO
No comments:
Post a Comment