Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 02, 2012

MAREKANI KUJENGA MITAMBO YA UMEME MTO RUHUJI MKOANI NJOMBE

Na Nickson Mahundi,Njombe.

Serikali ya Tanzania kupitia shirika la umeme tanesco,kwa kushirikiana na mwekezaji kutoka nchini marekani, inajiandaa kutekeleza mradi wa umeme wa maji katika mto ruhuji.

Akizungmza jana  kwenye baraza la madiwani, mpimaji ardhi   mwandamizi wa shirika la tanesco makao makuu Hamis Boby alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika hadi kufikia mwaka 2019 na kuzalisha umeme wa megawati takribani mia tatu hadi mia nne.

Bw.Boby alisema mradi huo utahusisha ujenzi wa mgodi wa kufua umeme wa megawati 350 hadi 500,bwawa la kuhifadhi maji ,bwawa la kuzalisha umeme,njia ya umeme,barabara,njia ya kusafirisha maji chini ya ardhi,ofis na makazi.

Hata hivyo alisema hatua hiyo itazingatia haki za wananchi katika eneo husika kwa kulipwa fidia ya ardhi,kupata huduma za kijamii,elimu ya mahusiano,pamoja na huduma nyingine zitakazopendekezwa kwenye makubaliano yao na wadau.

Akizungumzia malalamiko kuhusu fidia kwa wananchi, mpimaji huyo wa ardhi   mwandamizi wa shirika la tanesco makao makuu alisema utaratibu wa kutoa malalmiko hayo utapitia kwenye uongozi wa vijiji kabla ya kupelekwa kwa mkurugenzi wa wilaya afisa ardhi na tanesco ambapo tanesco na wataalam wa halmashauri watashughulikia malalamiko hayo.

Kwa upande wao madiwani wa halmashauri ya Mji Njombe na wilaya Njombe waliupongeza mpango huo wa serikali na kuwataka wawekezaji hao kutoa fidia kwa wananvhi wa maeneo husika bila kujali dini kabila wala rangi.

Akifunga kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Venancy Kabelege aliwataka madiwani kushirikiana na serikali katika kuwahamasisha wananchi ili kufanikisha zoezi hilola mradi.

Mwisho.



No comments: