Na Nickson Mahundi,Ludewa
Mvutano wa wanasiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi umezidi
kushika kasi katika chaguzi mbalimbali za chama hicho nchini mbapo jana katika
wilaya ya Ludewa mvutano huo uliendelea katika nafasi ya Halmashauri kuu ya CCM(NEC).
Katika mvutano huo wilaya Ludewa wagombea walionekana
kugongana katika matokeo ya uchaguzi kwa ngazi ya NEC ndipo wajumbe
walipotakiwa kurudia kwa mara ya pili ili kufanikisha kumpata mwakilishi kutoka
wilayani humo
Wagombea wa NEC walikuwa watatu ambao ni Bi.Elizabeth
Haule,Bi.Angera Libato na Mhandisi.Zefania Chaula lakini mvutano mkali ulikuwa
kwa wagombea wawili ambao ni Elizabeth Haule na Zefania Chaula kwa kugongana
matokeo yao ya kura za awali
Lilipo rudiwa zoezi la upigaji kura ndipo Bi.Elizabeth Haule
aliibuka mshindi kwa kura 592 na kuwa mwakilishi wa NEC huku mhandisi Zefania
Chaula akipata kura 452 akishindwa kuamini kuhusiana na matokeo hayo na
kutokukubaliana nayo.
Mhandishi Chaula alilalamikia kutotendewa haki katika
uchaguzi huo na kusisitiza mbele ya wajumbe kuwa atafuata ngazi husika na
kuyapeleka malalamiko yake ili kutambua ukweli wa matokeo hayo kwa kanuni ya
katiba ya CCM.
Aidha msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo Bw.Valensia Kabelege
aliwaambia waandishi wa habari kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki kama
ilivyotakiwa katika kanuni za chama cha mapinduzi na kumtaka mhandisi Chaula
kufuata ngazi za kisheria kama hakuridhika na matokeo hayo.
“uchaguzi umekwenda vizuri kama ilivyotakiwa ufanyike na
kama kuna mtu yeyote hajaridhika na matokeo haya basi anaweza kufuata ngazi
husika ili kutoa vielelezo vitakavyoonesha mapungufu yaliyojitokeza”,alisema
Bw.Kabelege.
Wengine walioshinda katika ngazi mbalimbali ni Felix Haule
katibu siasa na uenezi,Halmashauri kuu ya wilaya kupitia wazazi ni Donald Mwalongo,Hilary
Nkwera,Mathei Mtweve na Stanley Gowele.
Mbunge wa zamani wa jimbo la Ludewa na Mkuu wa wilya ya
Tarime mstaafu Bw.Stanley Kolimba alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Ludewa,wajumbe mkutano mkuu wa taifa ni,Monika Mchilo,Stanley Gowele,Leodiga
Mpambalyoto,Elisha Haule na Adalubeti Mgimba.
Waliochaguliwa mkutano mkuu wa Mkoa ni Selina Haule,Donald
Mwalongo na Oigeni Lugome aidha uchaguzi huo ulimalizika majira ya saa sita
usiku ndipo matokeo hayo yalipotangazwa na wajumbe kurejea vijijini kwao.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment