Umoja wa jumuiya ya Wanawake wa cha cha mapinduzi Tanzania UWT kwa
mkoa wa Njombe jana umefanya uchaguzi wa viongozi katika ngazi mbalimbali za
viongozi wa mkoa ambapo katika uchaguzi huo Rose Mery Lameck Lwiva aliweza
kumubwaga scolastika christian Kevela kwa kupata kura 190 kwa 164 kati ya
wapiga kura 354.
Miongozi mwa nafasi za uongozi zilizowaniwa na wagombea wa umoja huo wa
wanawake ni pamoja na nafasi ya mwakilishi UWT kwenda umoja vijana ccm mkoa wa
Njombe,mkutano mkuu wa ccm mkoa,mkutano mkuu wa taifa,umoja wa wanawake kwenda
wazazi mkoa na baraza la mkoa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa na Njombe Deo Sanga ambaye ni mbunge wa Jimbo
la Njombe Kaskazini amesema matokeo hayo yasilete mgawanyiko katika chama ili
kuepusha upinzani kushika dola mwaka 2015.
Rose mary ashukuru usimamizi ulivyofanyika vizuri hadi kupelekea ushindi mnono
kwake haku akieleza jitihada zilizofanywa na mwenyekiti anayemaliza muda sasa
kwa kipindi chote.
Awataka Madiwani kushikamana kuujenga mkoa wa Njombe huku akiahidi kuwa
sambamba na akinamama katika kujenga chama.
Katibu wa ccm mkoa wa Njombe bwana Hosea Mpagike asema Rufaa iko wazi kwa muda
wa siku 14 Kama yupo mwenyemalalamiko
Mama scolastika kevela asema kura 164 alizozipata ni kuwaheshimu akinamama wa
UWT huku akimtupia lawama mshindi kuwa siku moja kabla ya uchaguzi aligawa
vitenge wilaya ya Makete pamoja na kufanya mambo mengi kikiwemo chakula.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment