Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe, Njombe Press Club NPC Leo
Kimefanya Uchaguzi wa Viongozi wa Muda wa Chama Hicho Ambapo Bazil Makungu
Amechaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa NPCkwa kushinda kwa kura 20 19 kati ya 20
zilizopigwa Huku Ellymathew Kika Akichaguliwa Kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kushinda
kura 8 na kuwabwaga wagombea wenzake watatu..
Akitangaza Matokeo ya Uchaguzi Huo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Huo Shaban
Lupimo Amesema Mwenyekiti wa Muda wa NPC Bazil Makungu Amepata Kura 19 Kati ya
Kura 20 Zilizopigwa Huku Kura Moja Ikiharibika.
Amesema kwa nafasi ya katibu wa chama hicho Ndg.Hamis Hassan Kassapa ameshinda
kwa kura 15 kati ya 18 zilizopigwa na tatu kuharibika kutokana na mgombea kuto
kuwa na mpinzani huku Lilian Mkusa akichaguliwa kuwa makamu Katibu.
Katika nafasi ya uhasibu Sunday Bavuga amechaguliwa mara baada ya kukosekana
kwa mpinzani huku Consolatha kihombo akichaguliwa kuwa makamu wake.
Kwa Upande Wake Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Huo Fedrick Siwale ametangaza Majina
ya Wajumbe wa Kamati Kuu Tendaji wa Njombe Press Club watakao ingia kwenye
kamati hiyo.
Wajumbe hao ni wale saba watakaokamilisha safu ya watendaji 13 wa chama hicho
ambao ni pamoja na Festus Pangan,Nickson Mahundi,Gabriel Kilamlya,Riziki
Manufred,Amos Kaposo,Martha sanga pamoja na Mercy James,
Awali Akizungumza Kabla ya Uchaguzi Huo Mgeni Rasmi Deo Haule
Filikunjombe Ambae ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Amewataka Waandishi wa Habari
Kufanyakazi Kwa Zingatia Maadili, Mipaka, Misingi ya Taaluma Yao Pamoja na
Kutumia Weledi Walionao.
Katika Hatua Nyingi Filikunjombe Ameahidi Kutoa Vifaa Kwa Ajili ya Ofisi ya
Waandishi wa Habari Zikiwemo Kompyuta Ndogo (Laptop), Printer na Scannaer
pamoja na vifaa vingine.
Akizungumza Kwaniaba ya Viongozi Waliochaguliwa Mwenyekiti wa NPC Bazil
Makungu Amewashukuru Wajumbe wa Chama Hicho na Kuwataka Kuwa na Ushirikiano
Kati Yao na Viongozi Waliowachagua Ili Kufanikisha Malengo ya Chama
Hicho.
Uchaguzi Huo Umehudhuriwa na Wageni Kutoka Chama cha Waandishi wa Habari wa
Mkoa wa Iringa ICP Akiwemo Katibu wa ICP Frank Leonald
..........................................................................................................................
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment