Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 10, 2012

MKOA WA NJOMBE WAFANYA KIKAO KWA MARA YA KWANZA


Kwa mara ya kwanza mkoa wa Njombe jana umefanya kikao cha Kamati ya ushauri ya mkoa [RCC]huku Halmashauri zote za mkoa wa Njombe zikiagizwa kuhakikisha zinayafikia malengo katika ukusanyaji  mapato yake ya ndani.

Kikao hicho kimehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa wakiwemo baadhi ya wabunge wa mkoa wa Njombe,makatibu wakuu wastaafu wa chama na serikali pamoja na Naibu waziri wa maji Dkt.Binilith Mahenge ambaye ni mbunge wa Makete.

Akizungumza kwenye kikao hicho mwenyekiti wa kikao Captain Mstaafu Assery Msangi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Njombe amesema kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na halmashauri hizo lakini hazinabudi kuhakikisha zinafikia malengo yaliyowekwa kwa maslahi ya wananchi.

Katika kikao hicho vitengo mbalimbali vimewasilisha taarifa za utekeleza wa shughuli za idara husika ambazo zimeweza kuchangiwa na wajumbe wa kikao hicho huku taarifa ya zoezi la Sensa ya watu na makazi likitajwa kufanyika vizuri katika mkoa wa Njombe mara baada ya kufanyiwa uhakiki.

Pamoja na mambo mengine wajumbe wakikao hicho wameridhia Hospitali ya mji wa Njombe ya Kibena kuwa hospitali ya mkoa kwa muda wakati maandalizi yakifanyika licha ya agenda hiyo kuwa na mvutano kabla ya makuliano.

Akizungumzia suala la tatizo sugu la maji katika maeneo mbalimbali mkoani Njombe Naibu waziri wa maji Dokta Binilith Mahenge ameahidi kufuatilia na kulipatia ufumbuzi tatizo la huduma hiyo katika mji wa Njombe.

Shirika la maendeleo la NJODECO Pamoja na NJOLUMA ni imetakiwa kufanyiwa uchunguzi ili kupata suluhu ya utata uliopo kwenye vyama hivyo hadi hivi sasa kwani kitendo cha watu wachache kutumia mali za umma kwa maslahi binafsi kimekemewa huku mkuu wa mkoa wa Njombe akimuagiza mwanasheria wake kulifanyia kazi.



 

No comments: