Na Nickson Mahundi,Njombe.
Ucheleweshaji wa fedha za
miradi ya maendeleo kutoka Serikali kuu imekuwa kikwazo kikubwa cha utekelezaji
wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri za Mkoa wa Njombe.
Tatizo hilo limezikumba Halmashauri nyingi nchini
kutokana na fedha hizo kutoletwa kwa wakati hivyo kuzifanya Halmashauri kupata
hati chafu wanapopita wakaguzi na kuona fedha nyingi zikiwa hazijatumika.
Hayo yalisema jana katika
kikao cha ushauri cha Mkoa wa Njombe(RCC) ambacho ni kikao cha kwanza tokea
mkoa huu uanzishwe na baadhi ya wakurugenzi wa Halmashauri wa wilaya mbalimbali
mkoani hapa.
Akilitolea ufafanuzi suala hilo Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapten Assery Msangi alisema
ofisi yake inalitambua hilo
na kusisitiza ataendelea kuiomba Serikali kuu kuzileta fedha hizo mapema ili
ziweze kutomika kwa muda unaofaa.
Kapten.Msangi alisema ifike
wakati Halmashauri ziibue na kubuni miradi itakayosaidia katika makusanyo ya
mapato ya ndani ili kukamilisha miradi kwa wakati kuliko kutegemea mapato ya
nje.
“tumekuwa na utamaduni wa
kutegemea mapato ya nje zaidi lakini ninachotaka mkoa wangu uwe wa mfano katika
ukusanyaji wa mapato ya ndani kwani kumekuwa na udhaifu mkubwa katika
ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri mbalimbali”,alisema Kapten Msangi.
Kuhusu mgawanyo wa mali
za mkoa mama wa Iringa wajumbe walilalamikia kutogawiwa chochote kutokana na
ujenzi wa mkoa huo ulifanyika na mkoa wa Njombe pia.
Lakini cha kushangaza Mkoa wa
Iringa haukufanya mgao wowote kwa mkoa wa Njombe hali hiyo iliwasikitisha
wajumbe na kuahidi kulifuatilia suala hilo
kwa kina ili kupata ufumbuzi.
Aidha kikao hicho kilipitisha
kupandishwa hadhi kwa Hospitari ya Kibena kuwa ya Mkoa ili kusogeza huiduma za
afya zenye hadhi ya mkoa na kuvutia waewkezaji katika mkoa mpya wa Njombe.
Hatua hiyo ilifuatia baada ya
kuonekana ukosefu wa fedha za ujenzi wa hospitari ya mkoa ambapo eneo la ujenzi
wa hospitari hiyo lilishaandaliwa kinachosubiriwa ni ramani na fedha za ujenzi
wa Hospitairi hiyo.
Kwa upande wa kilimo Mkoa wa
Njombe ulionekana kuwa na wafanyabiashara wengi wanaotoka nchi ya Kenya
na kwenda moja kwa moja kwa wakulima ambao huwarubuni kwa kununua viazi kwa
rumbesa.
Hali hiyo iliwafanya wajumbe
kuhoji ujenzi wa soko la kimataifa katika mji wa Mkambako ambalo limeongelewa
kwa miaka mingi bila ya utekelezaji hali hiyo ndiyo inayosababisha biahsra ya
lumbesa.
Akizungumza kuhusiana na soko
hilo Mbunge wa Makambako Bw.Deo Sanga(Jaa
people) alisema ni muda sasa wananchi wa Makambako alikataliwa kuyaendeleza
maeneo ya soko hilo
lakini hakuna utekelezaji.
Kapten Masangi aliahidi
kulifuatilia hiyo kwa uwepo wa soko la kimataifa katika mkoa wa Njombe ni
ukombozi mkubwa kwa wakulima kutokana na kukoa huo kuwa na kilimo cha mazao
mbalimbali.
Changamoto kubwa ya mkoa huo
ilionekana ni upungufu wa wafanyakazi katika sekta mbalimbali,uchomaji
misitu,uhaba wa maji safi na salama na ukosefu wa soko la uhakika la mazao kwa
wakulima.
Hata hivyo kukao hicho
kiliazimia kuandaa ufunguzi rasmi wa mkoa huo ili kuwapa fulsa wadau mbalimbali
kutambuana na kuwakaribisha wawekezaji katika masuala ya kilimo ikiwemo ujenzi
wa viwanda vya kusindika mazao.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment