Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 10, 2012

VISIMA VYA MAFUTA NJOMBE VYAKOSA DIESEL TENA


Ikiwa ni siku chache baada ya kupatikana kwa mafuta aina ya petrol  kwenye vituo vya mafuta mjini Njombe adha hiyo imejitokeza kwa mara nyingine kwenye mafuta aina ya diesel huku vituo vingine vimeonekana kufungwa kwa muda tatizo ambalo limesababisha wafanyakazi wake kukosa kazi ya kufanya na kujikuta wakiishi bila kazi.

Baadhi wa wahusika wa vituo mbalimbali vya mafuta wameeleza sababu ya kukosekana kwa mafuta kuwa ni kuchelewa kufika kwa bidhaa hiyo ambapo sababu moja wapo walisema ni miundombinu mibovu hali inayosababisha ajari za mara kwa mara  na kusababisha uharibifa wa mali,


Aidha hali hii inasababisha pato la Taifa na la mtu mmojmmoja kushuka kwa asilimia kubwa,


Akiongea kwa niaba ya Meneja wa kituo cha mafuta cha Gapco Bi.Maria Msigwa amesema kwa upande wao tatizo hasa ni madeleva kushindwa kupakia kutokana na kuchelewa kwa oda,


Aliongezea kwa kusema kuwa kipindi kilichopita tatizo lilikuwa ni bei  ambapo alisema walikuwa wakinunua bidhaa kwa bei ya juu lakini kabla bidhaa hiyo kuisha bei inashuka na kusababisha hasara kubwa katika kampuni.


Wakiongea na mtandao huu wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com Baadhi ya  wananchi wa mkoa wa njombe wametupia lawama mamlaka husika kwa kusema kuwa haikuwekea mkazo swala zima la bei ya bidhaa hiyo.

No comments: