Na Nickson Mahundi,Ludewa
Wananchi wilayani Ludewa wametakiwa kujiandaa na ujio wa
wageni zaidi ya laki sita ambao watakuja katika machimbo ya migodi mikubwa ya
Mchuchuma na Liganga iliyoko wilayani humo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha
jana katika ufunguzi wa kikao cha kamati ya Ushauri(DCC)cha wilaya ya Ludewa
kutokana na mashirika na wageni mbalimbali kuanza kuingia katika wilaya hiyo
iliyoko jirani na nchi ya Malawi.
Bw.Madaha alisema shirika la maendeleo la Taifa(NDC) limeandaa
mpango wa uwezeshaji shirikishi kwa wananchi wa wilaya hiyo ili kuwaandaa
wananchi hao katika shughuri mbalimbali za ualishaji mali na kuwawezesha kutoka
katika wimbi la umaskini.
Alisema shirika la maendeleo la Taifa limemuandaa mtaalamu
kutoka nchini Afrika Kusini kuja katika wilaya ya Ludewa ili kuandaa mpango
mkakati wa maendeleo na elimu shirikishi kwa wananchi ili kupunguza migogoro
kati ya wawekezaji na wananchi na kuwapa fulsa ya kujitambua.
“NDC imempata mtaalamu kutoka nchi ya Afrika kusini kuja
hapa kuuandaa mpango wa maendeleo hivyo nawaomba wananchi kujiandaa na ujio wa
wageni kwani kutakuwa na changamoto kubwa kutoka kwao”,alisema Bw.Madaha.
Aidha aliwataka wananchi kujiandaa na zoezi la utoaji maoni
katika katiba mpya kwani zoezi hilo katika wilaya ya Ludewa linatarajia
kufanyikakuanzia tarehe 8 hadi 13 october mwaka huu katika maeneo mbalimbali.
Bw.Madaha alisema katika zoezi la maoni ya katiba mpya ni vema wananchi wakatoa maoni kwa kutumia
akili yao na si kwa utashi wa mtu mwingine, chama chochote cha siasa au Dini
kwa katiba ni muhimu kwa kila mtanzania.
Hata hivyo Bw.Madaha aliwapongeza wananchi kwa kushiriki
vema katika zoezi la Sensa ya watu na makazi kutokana na zoezi hilo kufanyika
vizuri katika wilaya ya Ludewa bila matatizo yoyote tofafauti na maeneo
mengine.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment