Na Nickson Mahundi, Ludewa.
Mbunge wa viti maalumu na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mh. Pindi Chana juzi alionekana kuhaha katika kuwapitisha watu wake katika ngazi mbalimbali wilayani Ludewa lakini juhudi hizo ziligonga mwamba baada ya kambi yake kushindwa.
Mh. Pindi alionekana akihangaika huku na kule ili kuhakikisha adhma yake inatimia kwa kuwashika wajumbe waliotoka katika kata mbalimbali kwaajili ya kupiga kura ili kuwachagua viongozi wa kiwilaya wa chama hicho huku akijitanda vitenge ili asionekane vizuri.
Juhudi hizo zilionekana kugonga mwamba katika ugawaji wa Mlungula kutokana na Taasisi ya kudhibiti na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya kazi kwa karibu katika ukumbi ambao uchaguzi huo ulifanyika.
Adhma ya Mh.Pindi ilikuwa ni kuwapitisha watu wake katika ngazi za uenyekini wa vijana wilaya,mwenyekiti wa wazazi wilaya na mwenyekiti wa UWT wilaya ambapo alionekana akimpikia debe mama Anna Mlowe kuwa mwenyekiti wa UWT.
Baada ya kufanyika uchaguzi huo Mkurugenzi wa uchaguzi wilaya ya Ludewa ambaye ni Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bi.Eva Degeleke aliwatangaza washindi na ndipo Mh.Pindi alipo pata hasira na kuondoka ghafra akielekea Iringa.
Walioshinda katika uchaguzi huo upande wa mwenyekiti wa vijana wilaya Bi. Elizabeth Haule, mwenyekiti wa wazazi wilaya Bw.John Kiowi na upande wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya alishinda Bi.Mary Mapunda.
Akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi wa uchaguzi Bi. Eva aliwataka wajumbe kuwa watulivu na kukubari matokeo wakati yakisomwa kwani chama ni kimoja hivyo hakuna haja ya malumbano zaidi ya kukijenga chama.
Bi. Eva aliwaomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kutumia busara walizotumia katika uchaguzi huo ili kufanikisha uchaguzi ujao wa kumchagua mwenyekiti wa wilaya wa chama hicho kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wametumia haki yao ya kikatiba ya chama kwa kumchagua wampendae.
Aidha ilitahadharisha kuwa na kampeni chafu kwa baadhi ya wanasiasa ndani ya chama cha mapinduzi ambazo hazileti tija kwani wanachama wa sasa wanauelewa mkubwa hivyo hawawezi rubuniwa na vijisenti kwa kuwachagua viongozi wasiofaa.
No comments:
Post a Comment