Na Nickson Mahundi.Njombe.
Mwenyekiti wa vijana kupitia Chama Cha Mapinduzi wilayani Ludewa
Bi.Elizabeth Augustino Haule (pichani chini) amepania kuwafanyia mambo makubwa vijana hao baada
ya kumchagua kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha miaka mnne kuanzia sasa na
kuendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Bi. Elizabeth alisema kutokana na yeye kuwa
mjasiliamali atatumia fulsa hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wilayani
humo kutoa elimu ya kujitambua kwani vijana walio wengi bado hawajitambui.
Alisema kama kijana anapaswa kijiajiri na si kusubiri kuajiriwa kwa
maisha bora kwa kila mtanzania hayaji kwa kutofanya kazi na kusubiri mtu au
kampuni ianzishe ndipo uajiliwe.
Bi.Elizabeth alibainisha kuwa mafanikio yake mpaka alipofikia kuwa
mwenyekiti ni juhudi binafsi na si mtu alikuwa nyuma yake kwani katika mikakati
yake ilikuwa kuwa diwani wa viti maalumu lakini bado lengo hilo
halijafikiwa na hajakata tamaa kwa hilo.
sija kata tamaa kwani naamini iko siku nitafikia malengo yangu kwa kujituma
hivyo napenda vijana wenzangu wajifunze kupitia mimi kwani penye nia pana njia
kila mmoja wetu akiamini hilo
atafanikiwa katika malengo yake",alisema Bi.Elizabeth.
Aidha amewataka vijana wa Chama Cha Mapinduzi kuto kukubari kurubuniwa na
wanasiasa kwa kuwa mgongo wao bali kuzingatia kanuni na sheria za chama hicho
katika kuwapata viongozi bora na kuendeleza juhudi za kukijenga chama.
Bi.Eliza alisema vijana kwa sasa wanahitaji elimu ya ujasilia mali na mitaji na si vinginevyo hivyo kama itaanzishwa Bank ya vijana itakuwa ukombozi mkubwa
kwani vijana wengi wataweza kupata mitaji na kufanya biashara zao.
Aliwaasa vijana wa wilaya ya Ludewa kutobweteka badala yake kujituma katika
kazi mbalimbali kwani kupitia migodi ya Mchuchuma na Liganga vijana wa Ludewa
wataweza kujikwamua kiuchumi na kuendesha maisha yao bila hofu.
Bi.Elizabeth alisema vijana wengi nchini wamekuwa ni watu wa kulalamika
badala ya kufanya kazi hiyo si busala kwani maisha bora kwa kila mtanzania
hayaji kwa malalamiko bali kwa kujitambua katika ufanyaji kazi za kujiongezea
kipato.
2 comments:
Very well written post. It will be valuable to anybody who utilizes it, as well as myself. Keep doing what you are doing – for sure i will check out more posts.
After research a couple of of the weblog posts on your web site now, and I truly like your means of blogging. I bookmarked it to my bookmark web site list and shall be checking back soon. Pls take a look at my site as nicely and let me know what you think.
Welcome to my blog [url=http://www.about-dogs.zoomshare.com/]www.about-dogs.zoomshare.com[/url].
Post a Comment