Na Nickson Mahundi,Njombe
Maafisa Ugani nchini wametakiwa kutoa taarifa sahii
Serikalini kuhusiana na maendeleo ya sekta ya Kilimo na mifugo kuanzia ngazi ya
Vijiji hadi kata ili kuiwezesha Serikali kupanga pajeti inayo stahili katika
wizara hiyo.
Hayo yalisemwa jana wilayani Ludewa na Kaimu mkurugenzi
msaidizi wa wizara ya Kilimo na Mifugo katika kitengo cha ufuatiliaji na
tathmini Bw.John Maige wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusu matumizi
ya fomu za kukusanyia taarifa za maendeleo ya kilimo na mifugo kwa maafisa
ugani wa vijiji na kata.
Bw.Maige alisema mafunzo hayo yanafanyika katika mikoa sita
ya nyanda za juu kusini ili kuwapa uwezo wagani kutunza kumbukumbu na kukusanya
taarifa katika mfumo mpya unaofadhiriwa na ASDPM &ETWG ili kupata takwimu
sahii toka kwa wakulima na wafugaji.
Alisema mradi huo umegawa pikipiki mbili kila wilaya na moja
kwa Hlmashauri za miji pia computer ili kuwezesha mchakato wa utunzaji
kumbukumbu,ufuatiliaji na tathmini kufanyika kwa urahisi kuanzia ngazi ya chini
na kuendelea.
“Tumeamua kutumia mfumo mpya kutokana na ule wa awali
kushindwa kukusanya taarifa kwa usahii hivyo tumegawa vitendea kazi ili
kurahisisha kazi hiyo ili tuweze kwenda sawa na mabadiliko ya sera ya kilimo
kwanza”,alisema Bw.Maige.
Awali mgeni rasmi akifungua mafunzo hayo ambaye ni kaimu
mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mhandisi.Baraka Mkuya alisema
wagani wanapaswa kuwezeshwa kwa kiasi kikubwa ili kuwafikia walengwa katika
maeneo ya jiji.
Mhandisi.Mkuya aliwataka wagani waliohudhuria mafunzo hayo
kuifanyia kazi elimu waliyoipata kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza adhma ya
Serikali katika ukusanyaji wa taarifa za kilimo na mifugo.
Aidha Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa(TAKUKURU)wilaya ya LudewaBw.Edings Mwakambonja aliwataka maafisa ugani
hao kufanya kazi kwa uadirifu kwani kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale
katika utendaji wao wakiwa vijijin.
Bw.Mwakambonja alisema wananchi wamekuwa wakiilalamikia
sekta hiyo kuhusika na kuchukua fedha kama kuchangia huduma pindi wanapohitaji
huduma ya matibabu ya mifugo au ushauri katika kilimo hasa maeneo ya mbali na
ofisi zao.
Alisema kama afisa ugani anapaswa kuwa mstari wa mbele
katika kupinga na kuikataa rushwa anapokuwa katika majukumu yake hivyo wakiona
kama kunadalili ya mfanyakazi mwenzao kuchukua rushwa nivema wakatao taarifa
mapema ili kuondoa sifa mbaya.
Bw.Maige aliwataka maafisa ugani hao kufanya kazi katika
mazingira yoyote kwani ni wachache nchini hivyo wanawakati mgumu kufika kila
kijiji kutokana na kutokuwa na vitendea kazi vya kutosha
Mwisho.
No comments:
Post a Comment