Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 16, 2012

MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA CCM LUDEWA AHAIDI KUFANYA MAKUBWA

Na Nickson Mahundi.Njombe.
Mwenyekiti wa vijana kupitia Chama Cha Mapinduzi wilayani Ludewa Bi.Elizabeth Augustino Haule (pichani chini) amepania kuwafanyia mambo makubwa vijana hao baada ya kumchagua kuwa mwenyekiti kwa kipindi cha miaka mnne kuanzia sasa na kuendelea.

 Akizungumza na waandishi wa habari jana Bi. Elizabeth alisema kutokana na yeye kuwa mjasiliamali atatumia fulsa hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wilayani humo kutoa elimu ya kujitambua kwani vijana walio wengi bado hawajitambui.

 Alisema kama kijana anapaswa kijiajiri na si kusubiri kuajiriwa kwa maisha bora kwa kila mtanzania hayaji kwa kutofanya kazi na kusubiri mtu au kampuni ianzishe ndipo uajiliwe.

 Bi.Elizabeth alibainisha kuwa mafanikio yake mpaka alipofikia kuwa mwenyekiti ni juhudi binafsi na si mtu alikuwa nyuma yake kwani katika mikakati yake ilikuwa kuwa diwani wa viti maalumu lakini bado lengo hilo halijafikiwa na hajakata tamaa kwa hilo.

sija kata tamaa kwani naamini iko siku nitafikia malengo yangu kwa kujituma hivyo napenda vijana wenzangu wajifunze kupitia mimi kwani penye nia pana njia kila mmoja wetu akiamini hilo atafanikiwa katika malengo yake",alisema Bi.Elizabeth.

Aidha amewataka vijana wa Chama Cha Mapinduzi kuto kukubari kurubuniwa na wanasiasa kwa kuwa mgongo wao bali kuzingatia kanuni na sheria za chama hicho katika kuwapata viongozi bora na kuendeleza juhudi za kukijenga chama.

Bi.Eliza alisema vijana kwa sasa wanahitaji elimu ya ujasilia mali na mitaji na si vinginevyo hivyo kama itaanzishwa Bank ya vijana itakuwa ukombozi mkubwa kwani vijana wengi wataweza kupata mitaji na kufanya biashara zao.

Aliwaasa vijana wa wilaya ya Ludewa kutobweteka badala yake kujituma katika kazi mbalimbali kwani kupitia migodi ya Mchuchuma na Liganga vijana wa Ludewa wataweza kujikwamua kiuchumi na kuendesha maisha yao bila hofu.

Bi.Elizabeth alisema vijana wengi nchini wamekuwa ni watu wa kulalamika badala ya kufanya kazi hiyo si busala kwani maisha bora kwa kila mtanzania hayaji kwa malalamiko bali kwa kujitambua katika ufanyaji kazi za kujiongezea kipato.
Enhanced by Zemanta

2 comments:

Anonymous said...

Very well written post. It will be valuable to anybody who utilizes it, as well as myself. Keep doing what you are doing – for sure i will check out more posts.

Anonymous said...

After research a couple of of the weblog posts on your web site now, and I truly like your means of blogging. I bookmarked it to my bookmark web site list and shall be checking back soon. Pls take a look at my site as nicely and let me know what you think.
Welcome to my blog [url=http://www.about-dogs.zoomshare.com/]www.about-dogs.zoomshare.com[/url].