Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

January 05, 2018

KUNDI LA WHATSAPP LA WILAYA YA LUDEWA LATOA MSAADA WA KITANDA HOSPITARI YA WILAYA.

 Bw.Obote Msemakweli akimkabidhi Dkt.Kilimba kitanda cha kubebea wagonjwa pamoja stand za drip
  baadhi ya Wanakundi la whatsapp la wilaya ya Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitari ya wilaya ya Ludewa

 Bw.Obote Msemakweli akimkabidhi Dkt.Kilimba kitanda cha kubebea wagonjwa pamoja stand za drip

 baadhi ya Wanakundi la whatsapp la wilaya ya Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitari ya wilaya ya Ludewa
  baadhi ya Wanakundi la whatsapp la wilaya ya Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Hospitari ya wilaya ya Ludewa
 hiki ndicho kitanda kilichonunuliwa na kundi la whatsapp la wilaya ya Ludewa
 Dkt.Kilimba wakiwashukuru wanakundi la wilaya ya Ludewa kwa kutoa msaada wa kitanda


Kundi la whatsapp lijulikanao kwa jina la wilaya ya Ludewa leo limetoa msaada wa kitanda cha kubebea wagonjwa katika hospitari ya wilaya ya Ludewa likiwakilishwa na wanakundi waishio Ludewa ambao nipamoja na Obote Msemakweli,Ocol Haule,Nickson Mahundi naSabinus Haule Digala ikiwa ni utaratibu wa kawaida waliojipangia wanakundi hao.

Akikabidhi kitanda hicho mmoja wa wanakundi hilo kwa niaba ya wengine Bw.Obote Msemakweli alisema kuwa kundi hilo linalojumuisha wanaludewa wanaoishi maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi limekuwa na utaratibu huo kila ifikapo mwisho wa mwaka kuchangishana na kutoa sadaka nyumbani.

Bw.Obote alisema kuwa michango ya wanakundi hilo la wilaya ya Ludewa imekuwa ikisaidia maendeo mengi ndani ya wilaya na hata nje ya wilaya kutokana na mahitaji kwani tayari kundi hilo lilishapeleka msaada katika hospitari ya Lugarawa,shule ya watoto wenye mahitaji maalumu Mundindi na maeneo mengine.

Alisema kuwa katika kundi la wilaya ya Ludewa kuna watu wenye uwezo tofauti wa kifedha hivyo inapotokea kuchangia jambo fulani kila mwanakundi huchangia kiasi ambacho anauwezo nacho,hivyo aliwataka watu mbalimbali kutumia mitandao ya kijamii katika kujiletea maendeleo.

"Leo hii tunakabidhi kitanda hiki cha kubebea wagojwa kikiwa na stendi nne za kutundikia madripu ikiwa ni michango wa wanaludewa wanaoishi maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi hivyo niwaombe uongozi wa hospitari ya wilaya kuvitunza vifaa hivi ili viwe msaada kwa wagonjwa",alisema Obote.

Naye Sabinus Haule Digala ambaye mmoja wa wanakundi hao akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa hospitari ya wilaya ya Ludewa Daktari Loth Kilimba majina ya waliochangia fedha za ununuzi wa kitanda hicho alisema kuwa kumekuwa na makundi mengi ya whatsapp ambayo hayana manufaa kwa wananchi hivyo ni wakati wa kujifunza kupitia group la wilaya ya Ludewa.

Akijibu baadhi ya maswali kwa wananchi waliohudhuria katika tukio hilo ambao walitaka kujua namna ya kujiunga la kundi hilo Bw.Digala alisema hakuna gharama yoyote ambayo mwanakundi anatakiwa kuilipia zaidi ya kushiriki pale linapotokea tatizo kama unahitajika mchango.

Akipokea kitanda hicho Mganga Mfawidhi wa hospitari ya wilaya ya Ludewa Daktari Loth Kilimba alisema kuwa mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kisiasa na katika mambo ya ajabu lakini mtandao unaotumiwa na wanaludewa umekuwa ni kimbilio na utatuzi wa matatizo kwa wenye shida.

Dkt.Kilimba alisema kuwa ifikie wakati mitandao hii itumike kama linavyofanya kundi la wilaya ya Ludewa kuona sehemu yenye mahitaji na kuweza kuchangia na kutatua changamoto zinazotokea kama hospitari na shule,hivyo kitanda hicho kitakuwa mapokezi ili kuwabebea wakonjwa walio katika hali mbaya ya standi za drip zitatumika katika wodi ya wajawazito.

Aidha Dkt.Kilimba alilipongeza kundi la wilaya ya Ludewa kwa kuikumbuka wilaya yao kwa kuchangishana fenda na kutatua changamoto za nyumbani pia aliwataka wanakundi kutoishia hapo badala yake kuangalia maeneo mbalimbali na ikiwezekana kufanya ziara ya pamoja wanakundi wote na kutembelea wilaya yao hasa maeneo ambayo wamewahi kutuo misaada.

mwisho.

No comments: