Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
leo tarehe 27 Oktoba, 2017 saa 8:00 mchana atawaapisha Makatibu Wakuu
wapya, Naibu Makatibu Wakuu wapya na Wakuu wa Mikoa wapya baada ya jana
tarehe 26 Oktoba, 2017 kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa
nyadhifa hizo.
- Ofisi ya Rais Ikulu.
- Katibu Mkuu – Bw. Alphayo Kidata
- Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
- Katibu Mkuu (Utumishi) – Dkt. Laurian Ndumbaro
- Naibu Katibu Mkuu – Dorothy Mwaluko (ATAAPISHWA)
- Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
- Katibu Mkuu – Mhandisi Mussa Iyombe
- Naibu Katibu Mkuu(Afya) – Dkt. Zainabu Chaula
- Naibu Katibu Mkuu(Elimu) – Bw. Tixon Nzunda
- Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
- Katibu Mkuu – Mhandisi Joseph Kizito Malongo (ATAAPISHWA)
- Naibu Katibu Mkuu – Bi. Butamo Kasuka Phillipo (ATAAPISHWA)
- Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
- Katibu Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) – Bw. Erick Shitindi
- Katibu Mkuu(Bunge na Waziri Mkuu) – Maimuna Tarishi
- Katibu Mkuu(Sera na Uratibu) – Prof. Faustine Kamuzora
- Wizara ya Kilimo.
- Katibu Mkuu – Mhandisi Methew Mtigumwe
- Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Thomas Didimu Kashililah (ATAAPISHWA)
- Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
- Katibu Mkuu (Mifugo) – Dkt. Maria Mashingo
- Katibu Mkuu (Uvuvi) – Dkt. Yohana Budeba
- Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
- Katibu Mkuu (Ujenzi) – Mhandisi Joseph Nyamuhanga
- Katibu Mkuu (Uchukuzi) – Dkt. Leonard Chamriho
- Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Dkt. Maria Sassabo
- Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Mhandisi Anjelina Madete
- Wizara ya Fedha na Mipango.
- Katibu Mkuu – Doto James Mgosha
- Naibu Katibu Mkuu (Utawala) – Bi. Susana Mkapa (ATAAPISHWA)
- Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) – Bi. Amina Shaaban
- Naibu Katibu Mkuu (Sera) – Dkt. Khatibu Kazungu
- Wizara ya Nishati.
- Katibu Mkuu – Dkt. Hamis Mwinyimvua
- Wizara ya Madini.
- Katibu Mkuu – Prof. Simon S. Msanjila (ATAAPISHWA)
- Wizara ya Katiba na Sheria.
- Katibu Mkuu – Prof. Sifuni Mchome
- Naibu Katibu Mkuu – Amon Mpanju
- Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
- Katibu Mkuu – Prof. Adolf F. Mkenda
- Naibu Katibu Mkuu – Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi
- Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
- Katibu Mkuu – Dkt. Florence Turuka
- Naibu Katibu Mkuu – Bi. Immaculate Peter Ngwale
- Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
- Katibu Mkuu – Meja Jen. Projest Rwegasira
- Naibu Katibu Mkuu – Balozi Hassan Simba Yahaya
- Wizara ya Maliasili na Utalii.
- Katibu Mkuu – Meja Jen. Gaudence Milanzi
- Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Aloyce K. Nzuki
- Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
- Katibu Mkuu – Dorothy Mwanyika (ATAAPISHWA)
- Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Moses M. Kusiluka
- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
- Katibu Mkuu – Prof. Elisante Ole Gabriel
- Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye (ATAAPISHWA)
- Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) – Prof. Joseph Buchwaishaija (ATAAPISHWA)
- Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
- Katibu Mkuu – Dkt. Leonard Akwilapo
- Naibu Katibu Mkuu – Prof. James Epiphan Mdoe
- Naibu Katibu Mkuu – Dkt. Ave-Maria Semakafu
- Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
- Katibu Mkuu (Afya) – Dkt. Mpoki Ulisubisya
- Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) – Bi. Sihaba Nkinga.
- Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
- Katibu Mkuu – Bi. Suzan Paul Mlawi (ATAAPISHWA)
- Naibu Katibu Mkuu – Nicholaus B. William (ATAAPISHWA)
- Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
- Katibu Mkuu – Prof. Kitila Mkumbo
- Naibu Katibu Mkuu – Mhandisi Emmanuel Kalobelo
Mhe. Rais Magufuli atawaapisha Wakuu wa Mkoa 6 aliwateua jana kama ifuatavyo;
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Manyara. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mnyeti alikuwa Mkuu wa
Wilaya ya Arumeru na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Joel
Bendera ambaye amestaafu.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Wangabo alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Nanyumbu na anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Zelote Stephen
ambaye amestaafu.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Geita. Kabla ya uteuzi huu Bw. Luhumbi alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Korogwe na anachukua nafasi ya Meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye
amestaafu.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Mara. Bw. Adam Kigoma Malima anachukua nafasi ya Dkt. Charles
Mlingwa.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bi. Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma Mjini na anachukua nafasi ya Bw. Jordan Rugimbana.
Mhe. Rais Magufuli atamuapisha Bw. Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara. Bw. Byakanwa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na
anachukua nafasi ya Bi. Halima Dendego.
Tukio la kuapishwa kwa viongozi hawa litarushwa moja kwa moja (Live)
kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam kupitia vyombo vya habari vya Redio na
Televisheni pamoja na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Oktoba, 2017
No comments:
Post a Comment