Mbunge mstaafu wa jimbo la Ludewa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Mzee Stanley Kolimba akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiyogo.
kulia ni Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ludewa mzee Stanley Kolimba,katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Edward Haule na anayefuata ni Makamu katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bw.Enzi Elias wakifuatilia jambo katika sherehe hizo
Makamu kati wa ccm wilaya ya Ludewa Enzi Elias akimkaribisha Mwenyekiti wa ccm wilaya ili aweze kuwahutubia wananchi
Viongozi wa ccm wilaya wakisalimiana na wachezaji wa timu za mpira wa miguu kutoka vijiji vya Lihagule na Kingole ambao walikuwa wakicheza fainali ya mashindano ya miaka 40 ya ccm wilaya ya Ludewa.
Viongozi wa ccm wilaya wakisalimiana na wachezaji wa timu za mpira wa miguu kutoka vijiji vya Lihagule na Kingole ambao walikuwa wakicheza fainali ya mashindano ya miaka 40 ya ccm wilaya ya Ludewa.
Makamu kati wa ccm wilaya ya Ludewa Enzi Elias akitambulisha ugeni kutoka wilayani
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa na diwani wa kata ya Ibumi Mh.Edward Haule akiwasalimia wananchi.
mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm Taifa mzee Thobias Lingalangala akifuatilia jambo
Ngoma ya asili ya Kihoda ya kijiji cha Kingole
kikundi cha Ngoma ya Asili ya Mganda ya kijiji cha Kiyogo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Haule akimkabidhi rambirambi mzazi wa mtoto ambaye aliuawa na Mamba katika mto Ruhuhu na mwili wake kutopatikana hadi leo.
Makamu kati wa ccm wilaya ya Ludewa Enzi Elias akitambulisha ugeni kutoka wilayani
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Haule akimkabidhi rambirambi mzazi wa mtoto ambaye aliuawa na Mamba katika mto Ruhuhu na mwili wake kutopatikana hadi leo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Haule akimkabidhi rambirambi mzazi wa mtoto ambaye aliuawa na Mamba katika mto Ruhuhu na mwili wake kutopatikana hadi leo.
Sherehe za
ccm wilaya ya Ludewa kutimiza miaka 40 zimeazimishwa kiwilaya katika kijiji cha
Kiyogo katika kata ya Masasi ikiwa ni moja ya mbinu za kusikiliza na kutafua
kero zinazokikabili kijiji hicho ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama tatizo
ambalo ni sugu kwa kijiji hicho wakati kitaifa sherehe hizo zimeazimishwa mjini
Dodoma.
Akitoa
hotuba mgeni rasmi katika sherehe hizo mbunge mstaafu ambaye ni Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa Mzee Stanley Kolimba alisema kuwa CCM ni
chama kilicholeta ukombozi Afrika hivyo kimekuwa kikiendelea kutatua changamoto
kwa wananchi wake kadiri muda unavyokwenda.
Mzee Kolimba
alisema changamoto kubwa zinazowakabili wananchi wa kijiji cha kiyogo ni pamoja
na ukosefu wa maji safi na salama,ukosefu wa nishati ya umeme pamoja na
miundombinu mibovu ya barabara na ndicho kilichowafanya viongozi wakapanga
sherehe hizo zikafanyika kijiji hicho.
Alisema
wananchi wa kijiji cha kiyogo wamekuwa wakihisi kuwa wametengwa na uongozi wa
wilaya kutokana na kutumia maji machafu kwa matumizi ya nyumbani ikiwa maji
hayo yamechafuliwa na wachimbaji madini katika vijiji vya Amani na vile vya
mkoa wa Ruvuma,lakini kiukweli Serikali inalijua hilo na tayari mbunge wa jimbo
ameanza kulifanyia kazi.
“Chama cha
mapinduzi na Serikali kwa ujumla inayatambua matatizo mliyo nayo hivyo mh.mbunge
wenu Deo Ngalawa anasema maji safi yanakuja pamoja na umeme pia uboreshaji wa
miundombinu ya barabara utafanyika mwaka huu hivyo msijihisi ni wapweke kuwa
mpakani huku.”,alisema Mzee Kolimba.
Awali
wananchi wa kijiji hicho walilalamikia kukosekana kwa miundombinu ya
kuunganicha kijiji cha Kiyogo na kijiji cha Kipingu kata ya Ruhuhu ili kuwapa
urahisi kupata huduma ya hospitari kubwa ya Lituhi katika wilaya ya Nyasa kwani
kivuko cha mitumbwi kimekuwa ni hatari kwao kutokana na mtu Ruhuhu kuwa na
Mamba wengi pamoja na Viboko.
Akijibu
swali hilo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa ambaye pia ni Diwani
wa kata ya Ibumi Mh.Edward Haule alisema kuwa mchakato wa kuunganisha kijiji
cha Kiyogo na kijiji cha Kipingu kwa Barabara utafanyika lakini hasa wananchi
wenyewe wanatakiwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo kwa kuanza kuichimba kwa
nguvu zao.
Mh.Haule
alisema kuwa vijiji vingi wilayani Ludewa vimeungana kwa kuanza kuchimba
barabara kwa nguvu zao hivyo wananchi wa Kijiji cha Kiyogo wanatakiwa kuianza
barabara hiyo ambayo ni fupi kuungana na kijiji cha Kipingu hivyo hata yeye na
wadau wengine pamoja na Diwani wa kata ya Masasi wanashiriki katika uanzishwaji
wa barabara hiyo kwani yeye ni mtaalamu wa barabara za vijiji.
Aidha makamu
katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ludewa Bw.Enzi Elias alisema kuwa ccm
imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watanzania wanaishi maisha mazuri
hasa katika kuhakikisha huduma za jamii zinapatikana kiurahisi hivyo vijana
wanatakiwa kuunda vikundi ili kuweza kupata mikopo itakayo wakwamua kiuchumi.
Bw.Enzi
aliwapongeza wananchi wa kijiji cha Kiyogo kwa kukiamini na kuendelea kuchangua
chama cha mapinduzi kuiongoza Tanzania kwani kijiji hicho hakuna kiongozi
yeyote wa upinzani ambaye ameweza kupewa nafasi kuanzia katika vitongozi hadi
kijiji wote ni ccm pia aliwataka kujiandaa na uchaguzi wa ndani ya chama na
kila mwanachama anahaki ya kugombea ili awe kiongozi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment