Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Ludewa Mh.Mery Mapunda akikabidhi vifutu mbalimbali kwa mlezi wa watoto yatima Lugarawa
wanachama wa UWT kata ya Lugarawa wilayani Ludewa wakiwa na viongozi wao wa wilaya
vitu mbalimbali vilivyokabidhiwa na uwt kwa watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Lugarawa wilayani Ludewa
Mtoto Vicent Mchilo(miezi 5)ni mmoja wa watoto walioacha na mama zao wakiwa wadogo,mama zao walifariki mara baada ya kujifungua.
Mwenyekiti wa UWT Ludewa Mh.Mery Mapunda akiwa na mtoto yatima
Katibu wa UWT wilaya ya Ludewa Bi.Maimuna Mwakaje akiwa anafuraha kumshika mtoto yatima Vicent Mchilo
Diwani wa kata ya Lugarawa Mh.Philomena Haule akiwa amempakata mtoto yatima
Viongozi pamoja na wanachama wa UWT Lugarawa wakifanya maandambano kutoka katika ofisi za kata mpka ktk kituo cha watoto yatima Lugarawa
Wanachama wa Uwt kata ya Lugarawa wakipata chakula baada ya kikao cha ndani
Umoja wa
wanawake Tanzania wa chama cha Mapinduzi(UWT)wilayani Ludewa katika mkoa wa
Njombe umeazimisha siku ya wanawake Duniani kwa kuwatembelea watoto yatima
katika kituo cha watoto yatima cha Lugarawa ambapo misaada ya vitu mbalimbali
imetolewa na umoja huo katika kituo hicho.
Akiongea na
walezi wa watoto yatima wa kituo cha Lugarawa Mwenyekiti wa UWT wilaya ya
Ludewa Mh.Mery Mapunda ambaye pia ni Diwani wa viti maalum kata ya Ludewa
alisema kuwa wanawake wa umoja huo
wameguswa wilayani Ludewa wameguswa na uwepo wa kituo hicho ambacho ni msaada
mkubwa kwa watoto yatima .
Mh.Mery
Mapunda alisema kuwa wao kama akina mama wanaujua uchungu wa mtoto hivyo ili
kuonesha kuwa wanajua kulea familia waliona ni vyema kwenda kutoa msaada kwa
watoto hao ambao ni wadogo kwa umri kwani wengine wanaumri chini ya miezi
mitano na waliletwa kituoni hapo baada ya mama zao kufariki dunia wakati
wakijifungua.
Vifaa
ambavyo vimetolewa na akina mama hao ni pamoja na Nguo,Sukari,Sabuni,Miswaki,Mafuta
ya kupakaa,Daftari,Penseli na maharange kwani kituo hivyo kinachosimamiwa na
Kanisa Katoriki Parokia ya Lugarawa jimbo la Njombe kimekuwa ni kituo cha
kwanza wilayani Ludewa chenye uwezo wapokea watoto wadogo wanaofiwa na mama zao
wakati wa kujifungua.
Naye katibu
wa UWT wilaya ya Ludewa Bi.Maimuna Mwakaje amewataka wadau mbalimbali ndani ya
wilaya ya Ludewa na Nje ya wilaya kuchangia misaada mbalimbali kwa watoto hao
kwani wanauhitaji mkubwa wa Sukari,Sabuni,mavazi na chakula kutokana na umri
waliokuwa nao.
Bi.Maimuna
aliwapongeza walezi wa watoto hao ambao ni watawa wa kanisa katoliki jinsi
ambavyo wanawatunza watoto hao kwa upendo wa hali ya juu kwani baadhi ya watoto
hao hawazijui sura za mama zao kutokana na mama zao kufariki muda mchache
wakati wakijifungua na kuwaacha watoto hao wakiwa hwana kumbukumbu za wazazi
wao.
“nawapokeza
walezi wote kwani tumefika hapa tumeona uhalisia wa watoto hawa wakiwalilia na
kutaka kubebwa na ninyi na hawahitaji kubebwa na watu wengine hivyo inaonesha
ni jinsi gani mnawajali na kuwapenda,sisi kama umoja wa wanawake wa chama cha
mapinduzi tumeona siku ya wanawake tuazimishe kwa kuwatembelea watoto hawa na
kutoa kidogo tulicho nacho”,alisema Bi.Maimuna.
Akishukuru
kwa niaba ya watoto hao na walezi wote Sister Koldula Mtewele OSB alisema kuwa
kuwa kituo hicho awali kilikuwa kikihudumiwa na wazungu,lakini kwa sasa
wamekabidhiwa wazawa baada ya wazungu hao kumaliza muda wao wa kuishi nchini na
kurudi kwao hivyo shukrani ziuendee UWT wilaya ya Ludewa kwa kuguswa na
changamoto zinazowakabili watoto hao.
Sister
Koldula OSB alisema kuwa watoto hao wanachangamoto nyingi hasa maziwa kwani
kuma mtoto mmoja anayeitwa Vicent Mchilo(5)ambaye mama yake alifariki akijifungua
na kumuacha anatumia kopo mbili za maziwa kwa wiki na nimaziwa maalum ambayo
huuzwa shilingi elfu ishirini na tano kwa kopo hivyo imekuwa ni shida pale
wanapokosa fedha ya kununulia maziwa hayo.
Alisema kuwa
kuna watoto wengine wanasoma awali na darasa la kwanza lakini wengine ni wadogo
mno ambao wanahitaji uangalizi wa karibu muda wote hivyo wanahitaji vyakula
muda wote,pia jamii inapaswa kuunga mkono jitihada za kituo hicho kwa kujitolea
vitu mbalimbali ambavyo vitasaidia ukuaji wa watoto hao ambao ni viongozi wa baadaye.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment