Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

November 19, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA LUDEWA ATOA SOMO KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE WILAYANI LUDEWA.


Katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Fortunatus Fungatwende akiangaliwa wanafunzi wakifanya upasuaji wa chura
 wanafunzi wa ST.Aloyse wakiingia ukumbini




Mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe MH.Deo Ngalawa amewataka wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne wilayani hapa kutokuwa na fikla za kuajiriwa na Serikali na badala yake wamalizapo vyuo vikuu kutengeneza ajira ambapo wataweza kuwaajiri wadogo zao wanaowafuata nyayo zao.

 Akiongea jana kwa niaba ya Mh.Ngalawa katibu wa mbunge huyo Bw.Fortunatus Fungatwende alipoalikwa kuwa mgeni rasmi katika shule ya Sekondari ya St.Aloyse inayomilikiwa na kanisa Katiliki Jimbo la Njombe iliyoko wilayani hapa alisema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wamekuwa wakiwa na mtazamo wa kuajiriwa na Serikali hali inayowafanya kuishi bila kazi wamalizapo vyuo vikuu. 

Bw.Fungatwende alisema kuwa ifikie wakati mwanafunzi anapokuwa anahitimu elimu yake awe na malengo ya kutengeneza ajira kwa wengine pia aliwataka wanaohitimu kidato cha nne kuwa na malengo ya kuendelea kimasomo na sio kuishia hapo kwali kidato cha nne ni kama elimu ya msingi kwa sasa.

 Alisema kuwa wilaya ya Ludewa inafulsa nyingi za uwekezaji lakini cha kushangaza vijana wanaotoka wilaya ya Ludewa hawataki kufanya kazi wilayani kwao na wanapohitimu masomo yao hubaki katika miji mingine wakilanda landa bila ya kazi waki Ludewa unaweza kufanya jambo na likakuingizia kipato na mwisho wa siku ukawaajili wengine.

 "inashangaza msomi unasubiri kuajiriwa wakati unauwezo wa kubuni mradi na kuwaajiri wengine kwani Mh.Ngalawa ameanza kutoa vitu mbalimbali katika vikundi zikiwemo mashine ambazo kikundi kinaweza kufanya uzalishaji wa unga na utotoleshaji wa vifaranga ni vitu ambazo unaweza ukawaajiri vijana wenzako na unaweza kujipatia fedha nyingi kwa wakati mmoja",alisema Fungatwende. 

 Alisema vijana walio wengi wilayani hapa wadai wanakimbia ugumu wa maisha hali ambayo sio kweli kwani tayari mbunge wa jimbo la Ludewa amefanikisha kuwepo kwa ,iradi mitano mikubwa ambayo itasababisha wilaya ya Ludewa kuwa namaendeleo ya haraka na kuzarisha ajira kwa baadhi ya vijana.

 Bw.Fungatwende alisema kuwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa daraja la mto Ruhuhu ambalo litaunganisha wilaya ya Ludewa na wilaya ya Nyasa na hivyo kuwafanya wananchi kufanya biashara baina ya wilaya hizo mbili,ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Lifua na Mkiu,ujenzi wa barabara ya lami kilomita 50,upatikanaji wa nishati ya umeme vijiji 49,uanzishwaji wa barabara ya mwambao wa ziwa Nyasa kuunganisha na wilaya ya Kyela na uanzishwaji wa viwanda vidogovidogo ambavyo vitazalisha ajira.

 Aidha aliwataka vijana kuipenda wilaya yao na wazazi kuitanguliza elimu mbele kwa kuwapeleka watoto wao shule ili wapate elimu ambayo itaweza kuwakomboa kimaisha kwani urithi wa mtoto sio Ng'ombe bali elimu itakayomsaidia katika maisha yake na familia yake. 

 Naye Meneja wa shule ya Sekondari St.Aloyse Padre Cathbeth Mlowe ambaye ni paroko wa Parokia ya Ludewa alisema kuwa shule hiyo inakabiliawa na changamoto ya upungufu wa nyumba za walimu na ukumbi wa chakula na mikutano richa ya kuwa ni shule inayoongoza katika ufaulu kwa wilaya ya Ludewa.

 Padre Mlowe alisema bado wazazi wa wilaya ya Ludewa hawana mwamko wa kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo hali inayosababisha wanafunzi walio wengi kutoka nje ya wilaya ya Ludewa hali hiyo pia imesababisha baadhi ya wasomi vijana wanaotoka wilaya ya Ludewa kutokuwa na uzalendo wa kufanya kazi wilayani kwao.

 mwisho.

No comments: