Mwenyekiti wa Ludewatinsmith Bw.Vianely Ngailo akiwaonesha waandishi wa habari mizinga ya Nyuki ambayo wameitengeneza tayari kwa kuigawa katika vikundi vingine
Katibu wa Ludewatinsmith Bw.Bahati Mtweve akionesha mizinga ya Nyuki
Mwenyekiti wa Ludewatinsmith Bw.Vianely Ngailo akitoa taarifa ya shirika lao
Prof.Ludwig Gernhardt akiongea na uongozi wa Ludewatinsmith
Bw.Willbad Mwinuka akiongea na uongozi wa Ludewatinsmith
Prof.Ludwig Gernhardt akiwaaga wanachama wa Ludewatinsmith
Vijana
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wametakiwa kuchangamkia Fulsa za
uwekezaji ili kwenda na wakati ambapo fulsa hizo ni pamoja na upandaji
miti,ufugaji wa Nyuki na Samaki pia kujiunga na vikundi mbalimbali ambavyo
vitawasaidia kupata mikopo kiurahisi.
Akiongea na waandishi
wa habari Ofisini kwake jana mwenyekiti
wa LudewaTinsmith group wilayani Ludewa Bw.Vianely Ngailo alisema kuwa Idadi
kubwa ya vijana wilayani hapa bado hawajitambui katika uwekezaji hivyo elimu
juu ya nini kifanyike kwa vijana inahitajika haraka iwezekanavyo ili kuwanusuru
vijana katika wimbi la umaskini.
Bw.Ngailo
alisema kuwa shirika la LudewaTinsmith lilianza kwa shida likiwa na idadi ndogo
ya wanachama lakini kwa kutambua fulsa za uwekezaji wilayani Ludewa limeweza
kujipanua na kufanya mambo makubwa ambayo yamekuwa ni msaada kwa vijana walio
wengi kwani mpaka sasa wanajitegemea katika maisha yao.
Alisema
kutokana na mipango waliojiwekea katika shirika lao wameweza kuaminiwa na wadau
mbalimbali na kupewa kazi kubwa kwani shirika hilo linajihusisha na utoaji wa
mafunzo ya ufundi uselemala,uungaji vyuma na ufundi magari ambao mpaka sasa
vijana wengi hujiunga katika shirika hilo kwa lengo la kunufaika na fulsa hilo
ambayo ni msingi wa maisha.
Bw.Ngailo
alisema kuwa hivi sasa wameweza kupata tenda kutoka kwa Prof.Ludwig Gernhardt ya kutengeneza Mizinga ya nyuki na tayari
wameshatengeneza mizinga 30 na kukikabidhi kikundi kingine cha vijana ambacho
kinajihusisha na ufugaji wa Nyuki kiitwacho ASHTECH GROUP chenye makao yake
wilayani Ludewa.
“Idadi kubwa
ya vijana wilayani Ludewa bado hawatambui fulsa zinazowazunguka ambazo zinaweza
kuwatoa katika wimbi la Umaskini,kwani sisi tulianza kwa shida lakini hivi sasa
tumekuwa na vijana wengi ambao tumewapatia mafunzo na tayari wanaendesha maisha
yao pia tumeanza kufanya kazi na vikundi vingine vya vijana kwa kuvichongea
mizinga kwa ufadhiri wa Prof.Ludwig Gernhardt kutoka nchi ya Ujerumani”,Alisema
Bw.Ngailo.
Naye katibu
wa shirika hilo Bw.Bahati Mtweve alisema kuwa kutokana na kazi wanazozifanya na
kutumia fulsa zilizopo wafadhiri kutoka mataifa mbalimbali Duniani yameanza
kuonyesha nia ya kutoa ufadhiri wa shirika hilo ili liendelee kuzalisha vinaja
ambao wataweza kuzitumia fulsa zinazowazunguka.
Bw.Mtweve
alisema mpaka sasa Prof.Ludwig Gernhardt
raia wa Ujeruman aliweza kulitembelea shirika hilo na kujionea kwa macho
kazi zinazofanywa na shirika la LudewaTinsmith ambapo alitoa ahadi ya
kuwasaidia vifaa vya kisasa zaidi vya ufundi Seremala ili waendendelee na
juhudi za kuzalisha vijana katika ufundi.
Alisema
licha ya Mjeruman huyo kutoa ahadi ya vifaa vya ufundi pia alilipatia shirika
hilo kazi ya kuchonga mizinga ya Nyuki na kukikabidhi kikundi kingine cha
vijana kijulikanacho kama Ash-tech group ambacho kinajishughurusha na ufugaji wa Nyuki,Samaki,upandaji wa miti na
uchimbaji wa visima ambapo mpaka sasa vijana hao tayari wameshakabidhiwa
mizinga 30.
Bw.Mtweve
alisisitiza kuwa wilaya ya Ludewa inafulsa nyingi za uwekezaji lakini bado
vijana hawana elimu ya Kutosha kuzitumia fulsa hizo hivyo kinachohitajika ni
mashirika mbalimbali yasiyo ya Kiserikali kuisaidia Serikali katika kuhamasisha
kundi la vijana kuchangamkia fulsa zilizopo.
Mwisho.
0762781393 mwenyekiti
0762781393 mwenyekiti
No comments:
Post a Comment