Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

June 22, 2016

VITUO VYA AFYA VYAPATIWA MSAADA





SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la SHIPO kwa kushirikiana na wafadhiri limetoa misaada wa vifaa vya huduma ya afya kwenye zahanati  Mkoani Njombe, 
 
Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 20 vimetolewa katika sekta ya afya, ambavyo vinakwenda kupunguza uhaba wa vifaa tiba katika zahanati ambapo vijiji vitano vitanufaika.

Meneja mkuu wa Shirika la SHIPO Oygen Mwalongo,akikukabidhi vifaa hivyo kwa serikali ya mkoa, ametoa wito kwa jamii kuacha kutegemea wafadhiri.
SB.Oygen Mwalongo-Meneja SHIPO
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr.Rehema Nchimbi akipokea n akukabidhi vifaa hivyo kwa vijiji vilivyopewa msaada huo ameagiza kuvitunza ili viweze kusaidia walengwa na kwa matumizi yaliyokusudiwa.
SB.dr.Rehema Nchimbi-RC Njombe
 
Upande wao wanufaika wanaeleza kuwa vifa hivyo kuwa vitasaidia kuondoa changamoto zilizokuwa zikiwakabili na kuongeza ufanisi wa kazi kwa kutoa huduma bora,Vijiji vilivyopata msaada vipo katika Wilaya ya Njombe,Ludewa,Wanging’ombe ambavyo ni Igodivaha,Igola,Ngalanga,Miva na Njelela.
 
 
NA  MERCY SEKABOGO
NJOMBE

No comments: