Baadhi ya majengo ya madarasa ya shule ya Morning Star Pre&Primary English Medium School
kibao cha shule
Lango la kuingilia Mornig Star Ludewa
Baadhi ya majengo ya madarasa ya shule ya Morning Star Pre&Primary English Medium School
Lango la kuingilia shuleni hapo
Baadhi ya majengo ya madarasa ya shule ya Morning Star Pre&Primary English Medium School
Baadhi ya majengo ya madarasa ya shule ya Morning Star Pre&Primary English Medium School
Wazazi
wilayani Ludewa mkoa wa Njombe wametakiwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto
wao tokea wakiwa wadogo kwa kuwapeleka watoto hao katika shule Binasfi ambazo
zinatoa elimu kwa Lugha ya Kingereza ili kuendana na soko la ajira Duniani
kwani bado mwamko wa elimu uko chini sana tofauti na maeneo mengine nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo mkurugenzi wa shule ya Morning star
Pre& Primary English Medium School wilayani hapa Bw.Maulid Mwingira alisema
kuwa bado wazazi wa wilaya ya Ludewa hawajawa na mwamko wa kutosha kuitumia
shule hiyo kutokana na mazoea waliyoyazoea ya kuwapeleka watoto wao katika
shule za msingi za Serikali ambazo hufundishwa kwa Lugha ya Kiswahili zaidi.
Bw.Mwingira
alisema kuwa shule ya Morning Star imekuwa shule pekee Ludewa mjini
inayojihusisha na utoaji wa elimu kuanzia darasa la awali kwa Lugha ya
Kiingereza kwani kabla ya shule hii
hapakuwa na shule nyingine katika mji wa Ludewa hali iliyokuwa ikiwafanya
baadhi ya wazazi wapenda elimu kuwapeleka watoto wao katika wilaya ya Njombe na
maeneo mengine.
Alisema
wakati umefika sasa kwa wazazi wa wilaya ya Ludewa kuwaandaa watoto wao katika
soko la Ajira kwa kuwapeleka Morning star ili waweze kujifunza Lugha ya
Kiingereza tokea wakiwa wadogo na kuacha mazoea ya kuwapeleka kuchunga ng’ombe
na kufanya vibarua wakisubiri umri ufike wakaanze darasa la kwanza katika umri
mkubwa shule za Serikali.
Bw.Mwingira
alisema shule yake ya Morning Star ilianza mwaka 2015 january na mpaka sasa
inajumla ya wanafunzi 99 wakiwemo wakike 47 na wakiume 52 ambapo elimu
inayotolewa hapo ni nzuri kwani wanapata mafunzo ya kompyuta pia hali ambayo
imekuwa ni kivutio kwa wazazi wengi wanaotoka wa maeneo tofauti na wilaya ya
Ludewa.
“Shule hii
ni ukombozi mkubwa kwa wanaludewa kwani awali walikuwa wanawapeleka watoto wao
wilaya za mbali na Ludewa kutafuta elimu lakini sasa tumewasogezea jirani
lakini cha kushangaza wilaya za Njombe na nyinginezo wanawaleta watoto wao
katika shule ya Morning Star lakini wazawa wa Ludewa bado wamekuwa wakusuasua
kuwaleta watoto wao,ushauri wangu kwenu tumieni fulsa hii ili kuendana na soko
la ajira pia kuwa na vijana wenye uwezo wa kuongea Lugha ya kiingereza na
wawekezaji wanaotarajia kuja Ludewa”,alisema Bw.Mwingira.
Naye Mwalimu
mkuu wa shule hiyo Boaz Kwenje alisema kuwa shule hiyo ni ya Bweni na kutwa
hivyo kwa wale wenye watoto wao majumbani ambao wanasoma na kurudi makwao huchukuliwa
na magari nyakati za asubuhi na kurudishwa jioni kwa uangalizi mzuri ambao
wazazi pamoja na watoto wao huufurahia kwani ni shule ya kwanza ambayo
haijawahi kuwepo katika mji wa Ludewa.
Mwalimu
Kwenje alisema kuwa shule hiyo ina walimu wa kutosha na wenye uzoefu
mkubwa hivyo inatangaza pia nafasi za
masomo kwa waliohitimu kidato cha nne ambao wanahitaji kupata mafunzo ya
kompyuta shule hiyo inawakaribisha kwa mwaka wa masomo 2017-2018 hivyo hivyo
kwa watoto wanaotaka kujiunga na madarasa ya Awali na darasa la kwanza pamoja
na la pili nafasi zipo.
Alisema kuwa
mpaka sasa wazazi wengi wamejenga imani na shule hiyo kutokana na ukweli
usiopingika kuwa Morning star inatoa elimu bora na isiyo na mashaka kwani
imekuwa ikishindana na shule nyingine za watoto katika mitihani na kushika
nafasi nzuri.
Mwisho.
Kwa
mawasiliano. 0756-654607/ 0759-238705/0764-279158.
No comments:
Post a Comment