Hizi ni motor za mashine hizo
Mashine zikishushwa ndani ya gari
Bw.Vasco Mgimba akichimba mtalo wa bomba za maji kutoka Ludende kuelekea Maholong'wa
katibu wa mbunge Bw.Fotunatus Fungatwende na Afisa wa ofisi ya Mbunge Bw.Victor Sanga wakishiri katika uchimbaji na ujenzi wa chanzo cha maji Ludende
mtungi wa gesi ambao ulinunuliwa na Mh.Ngalawa mbunge wa jimbo la Ludewa
hizo ndizo dawa zilizonunuliwa na Mbunge zikiwa katika zahanati ya Maholong'wa
Mbunge wa
jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh:Deo Ngalawa amewataka wananchi
wilayani Ludewa kuunda vikundi ili kuweza kunufaika na fulsa zinazozitokeza
hasa mikopo kwani bado wananchi wilayani hapa hawana utamaduni wa kuunda
vikundi hali inayowafanya kujikita
katika wimbi la umasikini.
Hayo
yamesemwa jana na katibu wa mbunge huyo Bw.Fotunatus Fungatwende wakati
akipokea mashine za kusaga,kukoboa na kukamua mafuta ya alizeti zilizotolewa na
Mh:Ngalawa zikiwa na lengo la kuvigawia vikundi mbalimbali ambavyo viliomba kwa
mbunge huyo.
Bw.Fungatwende
alisema kuwa Mh.Ngalawa anamalengo makubwa ya kuinua uchumi wa wapiga kura wake
lakini hataweza kutoa msaada kwa mtu mmoja mmoja lakini atatoa kwa vikundi
ambavyo vimeundwa na wananchi wenyewe wakiwa na lengo kujiinua kiuchumi.
Alisema kuwa
huo ni mwanzo tu kwa vikundi vilivyoundwa awali katika kata mbalimbali lakini
ataendelea kutoa vitu mbalimbali katika vikundi ili wananchi waweze kuwa na
miradi endelevu itakayowasaidia kujiinua kiuchumi kwani kwa kufanya hivyo jamii
itanufaika na miradi hiyo na anaamini itakuwa endelevu tofauti na kumuwezesha
mtu mmoja mmoja.
Bw.Fungatwende
alisema kuwa Mh.Mbunge wa jimbo la Ludewa ameona fulsa nyingi ambazo zinaweza
kuwa vyanzo vya mapato kwa wananchi wa Ludewa lakini wakitaka kunufaika na
fulsa hizo ni kujiunga katika vikundi na kuibua miradi yenye tija katika jamii nay
eye kama mbunge wao atawaunga mkono katika juhudi hizo.
“Mashine
hizi zinakwenda katika kata na vijiji mbalimbali katika wilaya ya Ludewa na
tutazigawa kutokana na maombi ya vikundi husika hivyo Mh.Mbunge ameshauri
wananchi kuendelea kuunda vikundi na kuibua miradi yeye kama mbunge wao
atawaunga mkono,mpango uliopo ni mkubwa ili kukuza uchumi Ludewa na hauwezi
kukamilika kwa kumsaidia mmoja mmoja hivyo ni vyema kutumia fulsa hii maana
wengine ndio wameanza kunufaika kupitia vikundi”,alisema Bw.Fungatwende.
Katika hatua
nyingine katibu huyo wa Mbunge aliweza kumuwakirisha Mh.Ngalawa katika
uchimbaji wa mtaro wa bomba ilikufanikisha maji safi na salama yanapatikana
katika kata ya Ludende kijiji cha Maholong’wa ambako awali aliweza kununua
mtungi wa gesi katika zahanati ya kijiji hicho ili kuweza kupasha moto vifaa
tiba.
Zahanati
hiyo ya kijiji cha Maholong’wa kata ya Ludende wilayani hapa imekuwa
ikikabiliwa na tatizo la mtungi wa gesi pamoja na jiko lake pamoja na dawa za kupunguza
maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa muda mrefu
hali iliyomlazim mbunge huyo kuvinunua vitu hivyo pamoja na dawa na kuukabidhi
uongozi wa kijiji hicho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment