Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

June 04, 2016

KITUO CHA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI CHAWAKARIBISHA WAZAZI WANAOTAKA KUWAPELEKA WATOTO WAO KITUONI HAPO.

 Mkurugenzi wa kituo cha NICOPOLIS ACADEMY Bw. Augustini Mwinuka


 Meneja wa NICOPOLIS ACADEMY Bw.Dancho Mwinuka
 wafanyakazi wa kituo hicho
  wafanyakazi wa kituo hicho



Kituo cha watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi wilyani Ludewa katika mkoa wa Njombe kijulikanacho kwa jina la NICOPOLIS ACADEMY kinawakaribisha wazazi wenye watoto wanaohitaji kupata elimu katika kituo hicho kwani kutokana na elimu bora inayotolewa kituoni hapo tayari baadhi ya wazazi wameshafanya hivyo.

Akizungumza na waandhishi wa habari jana ofisini kwake mkurugenzi mtendaji wa NICOPOLIS ACADEMY Bw.Augustino mwinuka alisema kuwa malengo ya kituo hicho ni kuwasaidia watoto yatima na waishio katika mazingira pia wale wenye ulemavu wa ngozi,lakini kutokana na ubora wa elimu unaotolewa kituoni hapo umewavutia baadhi ya wazazi ambao wamewapeleka watoto wao kwa kuchangia gharama kidogo.

Bw.Mwinuka alisema kuwa kutokana na wazazi hao kuwapeleka watoto wao ili wapate elmu uongozi wa kituo hicho umeona ni vyema kuwatangazia wananchi wenye watoto wadogo majumbani kuwapeleka watoto wao ili waweze kupata elimu na kuchangia kidogo katika gharama za uendeshaji kwani hata watoto wenye uhitaji na ambao walengwa watafarijika pale wanapoona wako na watoto wenzao wakitokea majumbani.

Alisema kuwa awali wazazi wengi walihitaji kupata fulsa hiyo kwa watoto wao lakini haikuwezekana kuwapokea lakini kutokana na kupokea ushauri kwa wataalamu mbalimbali uongozi umekaa chini na kuruhusu wazazi kuwaleta watoto wao ambao watakuwa wakipata masomo na nyakati za jioni kurudishwa makwao.

“malengo ya kituo cha nicopolis academy ni kwaajili ya wenye mahitaji maalumu kama wenye ulemavu wa ngozi na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi lakini kwa sasa tumeanza kuwapokea watoto wote lakini hawa wenye wazazi wao watachangia gharama kidogo pia tumeshauliwa kuchanganya ili hawa walengwa wasijihisi upweke”,alisema Bw.Mwinuka.

Bw.Mwinuka alisema kuwa yeye pia ni mfano kwa watoto wake tayari wanapata elimu katika kituo hicho hivyo mtanzania yeyote kutoka mkoa wowote anakaribishwa kuleta mtoto wake katika kituo cha NICOPOLIS ACADEMY kilichoko Ludewa mjini.
 Kwa mawasiliano piga no.0765059184

No comments: