Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein anaondoka leo jioni kwenda Muungano wa Visiwa vya Comoro kwa ziara ya siku mbili.
Akiwa
nchini humo Dk Shein atamuwakilisha Rais Dk John Magufuli katika
sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Azali Assoumani
Boinakher.
Kuapishwa
kwa Boinakher kunafuatia ushindi wake alioupata katika uchaguzi mkuu wa
nchi hiyo uliofanyika tarehe 10 Aprili 2016 na ule wa marudio katika
kisiwa cha Anjouan uliofanyika tarehe 11 Mei, 2016.
Sherehe
hizo za kuapishwa Rais huyo mteule zitafanyika kesho katika kiwanja cha
Mpira cha mjini Moroni na zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali kutoka nje ya nchi hiyo.
Katika
ziara hiyo Dk Shein amefuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Bora , Issa Haji Ussi Gavu na Mshauri
wa Rais Uhusiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia
Abdiwawa.
No comments:
Post a Comment