Aina ya ndizi zilizopo Mundindi wilaya Ludewa
Aina ya ndizi ambazo hulimwa nchini Mexico sasa zinapatikana Mundindi wilayani Ludewa
miembea na maembe makubwa yanayofikia kilo mbili yanapatikana Mundindi wilayani Ludewa
bwawa la samaki aina ya Sato
Nguruwe wa Kisasa walioko Mundindi
mbegu ya ndizi kutoka Mexico
Wananchi
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameanza maandalizi ya ufugaji wa samaki
na kilimo cha matunda mbalimbali kwaajili ya wawekezaji ambao wanaotarajia kuja
wilayani hapa kufanya kazi katika migodi ya chuma cha Liganga na Makaa yam awe Nchuchuma
miradi ambayo imekuwa ikitajwa kila kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu na
bila utekelezaji.
Akiongea na
mwandishi wa habari hizi katika kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa Padre
Melodious Mlowe ambaye ndio mfao wa wakulima na wafugaji wilayani hapa alisema
kuwa ili kujiandaa na uwekezaji wananchi wanapaswa kuandaa mashamba yao na
ufugaji wa kisasa bila kujali miradi hiyo inatarajia kutekelezeka lini.
Padre Mlowe alisema
kuwa yeye ameshajiandaa kwani mpaka sasa ameshafungua mashamba ya matunda
mbalimbali yakiwemo machungwa,maembe,Parachichi hufikia uzito wa kilogram tatu na ndizi kutoka vyuo vya
utafiti wa kilimo vya ndani ya nchi na nje ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa
yameshaanza kupata soko katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa na nje ya mkoa.
Alisema kuwa
anazaidi ya hekali 20 za matunda ambapo
kwa upande wa ndizi kuna migomba ambayo aliitoa mashamba ya kilimo ya Serikali
Bihalamulo,chuo cha kilimo SUA Morogoro,Ruanda
na Burundi ambayo ni aina maalumu na inazalisha kwa wingi pia kuna migomba
ambayo inazaa ndizi za mapambo lakini zinaliwa kama kawaida kutoka nchini
Mexico.
Kwa upande
wa Parachichi ana aina ambayo aliitoa nchini India pia michungwa na miembe
ambayo aliitoa katika chuo cha SUA ikiwa ni malengo yake ya kuwagawia wananchi
ili waweze kufanya kilimo cha matunda hayo ili kuweza kuwalisha wageni ambao
wataajiliwa katika miradi hiyo miwili mikubwa inayotarajia kuanza.
“Nimefungua
mashamba makubwa na kutafuta mbegu zilizofanyiwa utafiti ili kuisaidia jamii ya
wilaya ya Ludewa kuanza kujiandaa na fulsa kwani baadhi ya wananchi wanafikiri
miradi hiyo itaweza kuwaajiri wananchi wote jambo ambalo sio sahihi hivyo
lazima kila mtu ajifunze kuzalisha kwa wingi ili itakapoanza miradi hiyo aweze
kujipatia kipato kwa kuwauzia wafanyakazi wa miradi hii”,alisema Padre Mlowe.
Padre Mlowe
licha ya kilimo cha matunda pia alisema kuwa ameweza kutengeneza mabwawa ya
samaki zaidi ya 25 ambayo yana samaki aina mbalimbali wakiwemo Sato na Pelege
wa bwawa la Mtela ambao tayari amekwishaanza kuwauzia raia wa China ambao
wanaendelea na maandalizi ya ujenzi wa viwanda katika migodi hiyo.
Alisema kuwa
ufugaji wa Samaki huo aliupata kutoka kwa watafiti wa samaki kutoka Mwanza
hivyo kila Bwawa linaaina yake ya Samaki kwa mwishoni wa mwa ka 2015 aliweza
kuwavua samaki na kuwagawia wananchi ili kuonja radha ya samakini hao ikiwa ni
moja ya ushawishi kwa wananchi ili waweze kujifunza ufugaji wa samaki hao ambao
wanaweza kuwa ni ukombozi mkubwa katika uchumi wao.
Vilevile
katika shamba hilo ambalo ni la mfano wilayani Ludewa kuna ufugaji wa
Bata,Kuku,Ng’ombe wa maziwa pamoja na Nguruwe kwani wawekezaji wa kichina hupendelea
vyakula hivyo ambapo ufugaji wake hautumii gharama kubwa kwani kuna baadhi ya
wananchi wameweza kufika katika shamba lake na tayari wameanza ufugaji huo
pamoja na kilimo cha matunda.
Aidha
aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kuendelea kujiandaa kuzalisha katika
uwingi bila kujali maneno ya kukatishwa tamaa kuwa miradi hiyo ya Chuma na
Makaa ya mawe ni hadhithi tu haiwezi tokea.
Mmoja wa
wananchi wa wilaya ya Ludewa Bw.Albetho Mwinuka alisema kuwa wananchi wa wilaya
ya Ludewa ni watendaji wazuri wa kazi lakini wamekuwa wakikatishwa tamaa na
Serikali kutokana na kushelewa kuanza miradi hiyo mikubwa ambayo ingeweza
kuinua uchumi wa Taifa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment